Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na WaterAid UK zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati ili kuendeleza huduma endelevu za Maji, Usafi wa Mazingira, na Usafi wa Binafsi (WASH).
Ushirikiano huo unalenga kuimarisha mifumo ya kitaasisi, kutekeleza miradi, na kupanua uwekezaji unaohimili mabadiliko ya tabianchi ili kuongeza kasi ya maendeleo ya sekta hiyo.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ambaye pia ni Gavana Mbadala (Alternate Governor) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, na Bw Robert Mtengule, ambapo kwa upande wa WaterAid UK, alikuwepo Mkurugenzi wa Pan Africa Advocacy, Dkt. Tanko Yussif Azzika na maafisa wengine wa Wizara ya Fedha.





