Featured Kitaifa

IGP WAMBURA APANGUA BAADHI YA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo ya  kuwahamisha baadhi ya Makamanda wa Polisi, ambapo amemhamisha Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa  Mbeya kwenda Makao makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa  Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Benjamini Kuzaga.  

Pia, IGP Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Katabazi kutoka  Makao makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara  kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Benjamini Kuzaga aliyehamishiwa  kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.  

Ndugu Wanahabari,  

Mabadiliko haya ambayo yalianza tarehe 08.09.2022 ni katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji  wa majukumu ya Jeshi la Polisi. 

Imetolewa na:  

About the author

mzalendoeditor