Featured Michezo

FIFA KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA, YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

Written by mzalendoeditor

Na John Mapepele
Rais
wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Gianni Infantino  amesema  FIFA
itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada
mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu
Hassan kwenye Michezo.
Akizungumza
usiku wa kuamkia leo Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja
cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia
Tanzania.
Akiongozana na
wachezaji mahiri wazamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na
mwamuzi  Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali
zinazofanywa na Tanzania.
“Tayari
FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga
lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine”
amefafanua Mhe. Mchengerwa
Aidha,
Mhe. Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada
kubwa kwenye ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika
michezo.
Mhe. Mchengerwa
amepokea viongozi mbalimbali wa juu kwenye mashirikisho ya Soka duniani
na kufanya  vikao vya kuendeleza michezo ambao leo wanahudhuria mkutano
Mkuu wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) jijini Arusha.
Aidha,
Mhe. Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuendelea kuimarisha mahusiano na
mashirikiano na nchi mbalimbali ambazo tayari ziliahidi kuendeleza
mashirikiano katika sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni.
Mkutano
huu wa kihistoria unatarajiwa kuhudhuria na zaidi ya watu mia tano na
waandishi wa habari zaidi ya mia moja huku ikitarajiwa kuangaliwa na
zaidi ya watu bilioni moja.
Tayari
viongozi  wakuu wa mashirikisho yote ya Soka kutoka mabara yote
wamewasili na Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa  anatarajiwa
kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu
Hassan.

About the author

mzalendoeditor