Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga akiwa na viongozi wa CCM Mkoa wa Rukwa Leo alipowasili rasmi mjini Sumbawanga ambapo amesema yupo tayari kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kuleta maendeleo kwa wananchi.

(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

…………………………

Na. OMM Rukwa 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Queen Sendiga leo (09.08.2022) amewasili katika Kituo chake cha kazi Mkoa wa Rukwa kufuatia kuteuliwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Mapema akiwa mjini Sumbawanga amesaini kitabu cha wageni katika Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Rukwa ambapo amewaeleza kuwa amekuja kufanya kazi kwa ustawi wa Wana Rukwa na Taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Rainer Lukala amemkaribisha kiongozi huyo na kumuahidi kuwa CCM itashirikiana naye kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Donald Nssoko kesho Agosti 10 Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa atakabidhiwa rasmi ofisi toka kwa mtangulizi wake Mheshimiwa Joseph Mkirikiti tukio litakalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Sumbawanga.

Mheshimiwa Sendiga anahamia Mkoa wa Rukwa kutokea Mkoa wa Iringa kufuatia uteuzi uliofanywa Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Previous articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 10,2022
Next articleFIFA KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA, YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here