Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFUNGUA BARABARA YA CHUNYA-MAKONGOROSI,CHUNYA MKOANI MBEYA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Chunya katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja Matundasi Wilayani humo Mkoani Mbeya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria ufunguziBarabara ya Chunya-Makongorosi km (39) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami katika sherehe zilizofanyika Matundasi Chunya Mkoani Mbeya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi Barabara ya Chunya-Makongorosi km (39) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami katika sherehe zilizofanyika Matundasi Chunya Mkoani Mbeya.

………………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na TAMISEMI kupitia Halmashauri zote nchini na kuhakikisha zinaweka mipango ya kukusanya mapato. 

Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Chunya -Makongolosi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 39 iliyofanyika katika uwanja wa Matundasi.

Aidha, Rais Samia amesema mapato yanayokusanywa na Halmashauri yakisimamiwa vizuri yanaweza kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Chunya mjini, Rais Samia ameagiza Madiwani na Wenyeviti wa eneo hilo wanaopata mapato mengi kutokana na kutoa leseni nyingi za biashara kujenga kituo cha mabasi cha Chunya.

Vile vile, Rais Samia ameeleza barabara hiyo itafungua fursa za kibiashara kwa wananchi wa Chunya kwani inaunganisha mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani. 

About the author

mzalendoeditor