Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI  JENGO LA OFISI YA RC MBEYA,AANZA ZIARA MKOANI MBEYA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbeya waliofika kwenye hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya zilizofanyika Jijini Mbeya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Mbeya 

Sehemu ya Wananchi waliohudhuria hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Mbeya

…………………………………….

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha huduma ya maji safi kwa wananchi katika miradi inayozinduliwa inakuwa endelevu. 

Rais Samia amesema hayo leo wakati akizindua Mradi wa Maji wa Shongo – Mbalizi mkoani Mbeya uliogharimu shilingi bilioni 3.345. 

Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara hiyo kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi inawafikia wananchi kwa uhakika kwa kuwa Serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo kwa manufaa ya wananchi. 

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa jengo la afya ya huduma ya mama na mtoto hospitali ya Meta ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia akina mama zaidi ya 300 litakapokamilika.

Ujenzi wa jengo hilo utakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia kina mama wa mkoa huo na kutoka mikoa mingine ya Nyanda za juu Kusini. 

Vile vile Rais Samia ameweka Jiwe la Msingi katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kuwataka madiwani mkoani humo kuhakikisha kuwa asilimia 10 ya Halmashauri inatumika katika miradi ya maendeleo. 

Rais Samia yuko mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

About the author

mzalendoeditor