Featured Kitaifa

WAZIRI MCHENGERWA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO SHULE ZOTE WILAYA YA RUFIJI,AANZISHA LIGI YA SENSA

Written by mzalendoeditor


Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji.  Mhe,
Mohamed Omary Mchengerwa ametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za
msingi na Sekondari na wanafunzi wanamichezo wote  wanaoshiriki kwenye
mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Mashindano 
ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2022 Wilaya ya Rufiji.
Mhe.
Mchengerwa amekabidhi  vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Julai
17, 2022 kwenye  shule ya Sekondari ya Ikwiriri   Wilaya ya Rufiji
ambapo amesema ameamua  kufadhili vifaa hivyo katika Wilaya ya Rufiji
ili kuiendeleza michezo kwa kuwa michezo ni biashara  na ajira kubwa 
kwa vijana.
“Nimeamua
kusaidia vifaa hivi kwakuwa natambua  kwa sasa michezo ni miongoni mwa
chanzo cha ajira na biashara kubwa duniani hivyo ni vema kufanya michezo
kwa umakini mkubwa ili kujipatia ajira” amefafanua
Amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu na kujituma kwa kufanya mazoezi ili waweze kushinda kwenye  mashindano mbalimbali.
“Nendeni
mkajitume, michezo ni ajira na  furaha wasikilizeni walimu wenu,  hata
shuleni  mtafanya  vizuri”amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Aidha
amesema dhamila ya Serikali kwa sasa  ni kuendeleza michezo ambapo
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu
Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya kwenye michezo  katika kipindi
kifupi cha utawala wake ambazo zimeleta  mapinduzi makubwa kwenye sekta 
hiyo.
Vifaa hivyo vimegharimu zaidi ya milioni 23 ambazo zimenunua zaidi ya jezi seti 200, trakisuti pea 100, kofia 200 na mipira 100.
Pia
amefadhili Ligi ya mpira wa miguu ya   sensa katika Wilaya ya Rufiji
ambapo ametoa seti 6 za jezi kwa timu sita na  mipira  12 kwa ajili ya
mashindano  hayo.
Amesema
lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha  wananchi  kushiriki
kuhesabiwa  kwenye sensa ya kitaifa  yam waka huu  kwa manufaa mapana ya
wananchi wa Rufiji na Taifa kwa ujumla.
Aidha,
amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Rufiji na watanzania wote kujitokeza
kwa wingi Agosti 23, mwaka huu kuhesabiwa kwenye zoezi la sensa kitaifa.
Mwenyekiti
wa Halimashauri ya Wilaya ya Rufiji amemshukuru Mhe. Mchengerwa  kwa
jitihada  zake  na mchango wake kwenye sekta ya michezo ambapo
amemhakikishia kuwa michango anayotoa itatumika vizuri ili  kupata
matokeo chanya.

About the author

mzalendoeditor