Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni wamefanya kikao cha pamoja na Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Shibru Kedida tarehe 06 Julai 2022 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili juu ya kuimarisha ushirikiano imara na wa kihistoria baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja na changamoto za uhamiaji haramu nchini.
Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Kulia ni Kamishna wa Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka wa Idara ya Uhamiaji, Samwel Mahirane akifafanua jambo juu ya masuala ya usimamizi wa mipaka wakati wa majadiliano ya kikao hicho, pembeni yake ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza nchini, ACP George Wambura.
Aliyesimama ni Naibu Kamishna Msaidizi wa Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka wa Idara ya Uhamiaji,Phabian Philo akifafanua jambo katika majadiliano ya kikao hicho.
Majadiliano yakiendelea.
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara hiyo wakaijadiliana jambo na Kamishna Mahirane na Kamishna Philo wa Idara ya Uhamiaji baada ya kumalizika kwa mazungumzo.
Picha ya Pamoja Waheshimiwa Mawaziri, Mhe. Balozi na Ujumbe walioambatana nao katika kikao hicho.
Waziri Mulamula akiagana na Mhe. Balozi Shibru Kedida baada ya mazungumzo.