Featured Kitaifa

MASHIRIKA 13 KUTOKA NCHI TATU ZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA ARUSHA KUJADILI NAMNA BORA YA KUZUIA UKATILI KWA WATOTO.

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya haki elimu Dkt John Kalage akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wao mkoani Arusha.
Kamishna wa ustawi wa jamii wa wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na makundi maalum Dkt Nandera Muhando akionyesha  kwa waandishi wa habari moja  kitabu cha muongozo walichokizindu katika mkutano wa wadau wa kupinga ukatili kwa watoto.
Baadhi ya wadau wa kupinga ukatili kwa watoto shuleni na nje ya shule kutoka nchi za Uganda, Tanzania na Kenya wakiwa katika mkutano wao wa sita mkoani Arusha.
………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mashirika 13 kutoka nchi tatu za  za Afrika Mashariki ya kupinga ukatili wa watoto mashuleni yamekutana mkoani Arusha katika mkutano wao wa sita  kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili namna bora ya kuzuia vitendo vya ukatili nje na ndani ya shule.
Akifungua mkutano huo wa kujifunza kwa vitendo afua mbalimbali ambazo zinafanywa na wadau wa Afrika mashariki kuhusu suala la ukatili wa watoto, Kamishna wa ustawi wa jamii wa wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na makundi maalum Dkt Nandera Muhando alisema kuwa takwimu za ukatili zimekuwa juu kulingana na taarifa za jeshi la polisi  za 2021/2022 ambapo wizara imeipa kipaumbele kwasababu ya nia yao ni kuwasaidia watoto walio shule na nje ya shule katika kuangalia usalama wao.
Dkt Muhando alisema Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ukatii katika maeneo mbalimbali nchini Serikali imezindua miongozo kitaifa wa uundaji na uendeshaji  wa mabaraza ya watoto Tanzania pamoja na madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto ndani na nje ya shule ambapo miongozo hiyo ni moja ya mikakati ya kusaidia kupunguza ukatili kwa watoto.
“Miongozo hii ni muhimu katika kuweza kutusaidia kuwafikia hao watoto lakini pia na wanawake kwani sisi tumepewa jukumu kubwa la kumlinda mtoto chini ya sheria namba 21 ya 2009 pamoja na marekebisho madogo ya mwaka huo ambapo tutamlinda katika makao mbalimbali,nyumba salama na walioko mitaani,Alisema Dkt Muhando. 
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa haki elimu Dkt John Kalage alisema mkutano huo umewakutanisha mashirika 13 kutoka Uganda,Kenya na Tanzania ambao ni mahususi kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali pamoja na ubadilishanaji wa uzoefu wa masuala ya kuzuia na ukatili kwa watoto ambao unafanyika nje na ndani ya shule.
“Tumeamua kubadilisha uzoefu ili shule ziwe salama kwa watoto kujifunza pamoja na kuwaondolea hofu pindi wanapoenda na kurudi shuleni kwani pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali bado vitendo hivyi vimekithiri katika baadhi ya maeneo mbalimbali,”Alieleza Dkt Kalage. 
Aidha alifafanua kupitia kukithiri kwa matukio ya ukatili kwa watoto na wanawake imepelekea kutafuta mbinu shirikishi kutoka katika nchi zilizoendelea ili kuweza kujifunza namna ya kuzuia kwa lengo la kupunguza vitendo hivyo katika jamii.
Dkt Kalage aliwataka wananchi kuendelea kufichua na kutaoa taarifa katika vyombo husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake dhidi ya mtuhumiwa na vitendo vya ukatili viweze kupungua na watoto waweze kuwa salama na kujifunza ipasavyo.
Naye Afisa ustawi wa jamii wa mkoa wa Arusha Denis Mgiye alieleza kuwa  anashukuru wadau kwa kushirikiana na serikali kuzindua miongozo hiyo iliyolenga katika kuhakikisha watoto wanalindwa lakini bado wanaendelea kupambana na masuala ya ukatili.
“Serikali kwa kushirikiana na wadau wanafanya juhudi katika kukabiliana na vitendo hivyo lakini changamoto ni baadhi  ya familia kumalizia kesi nyumbani hali ambayo inachangia kuongezeka kwa matukio hayo,”Alisema.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo,Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya Arusha,Angela Mvaa amesema wamekuwa wakikabiliana na vitendo vya ukatili kwa kushirikiana na jamii 

About the author

mzalendoeditor