Featured Kitaifa

UTEUZI:RAIS WA ZANZIBAR DK.MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi, Juni 24, 2022 amefanya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali uongozi. 

Rais Mwinyi amemteua Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Anakaimu wadhifa wa Jaji Mkuu wa Zanzibar.

Pia, awateua Ndugu Salma Ali Hassan, Mohamed Ali Mohamed, Said Hassan Said kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Aidha, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Salum Kassim Ali kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, ambapo kabla ya uteuzi huo Ndugu Salum alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kusini Unguja.

Ndugu Ali Salim Ali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ukimwi Zanzibar ambapo kabla ya uteuzi Ndugu Ali alikuwa ni mshauri wa masuala ya ukimwi katika jumuiya ya ZAPHA+

About the author

mzalendoeditor