Burudani Featured

HARMONIZE AMVISHA PETE YA UCHUMBA KAJALA MASANJA

Written by mzalendoeditor

MSANII wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ’Harmonize’ kumvalisha pete ya uchumba msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja.
Tukio hilo limefanyika leo Jumamosi Juni 25, 2025 hoteli ya Serena na kulipa jina la ‘Late Lunch’ huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang, Mkurugenzi wa TV E, Francis Ciza ’Majizo’.
 Harmonize amesema wamepitia mengi na msanii huyo na anashukuru hatua hiyo waliyofikia.
Aidha amesema kwa wasiojua yeye na Kajala wamejuana zaidi ya miaka saba iliyopita tangu akiwa hana pa kulala mpaka kupata mafanikio aliyonayo leo.
“Mimi na Kajala tuna historia ndefu, tulijuana miaka saba iliyopita nililala kwake nikiwa sina pa kulala mpaka leo mnaponiona hapa,” amesema Harmonize

Kwa upade wake Kajala ammesema “Hakuna asiyejua tuliyoyapitia, pia mimi sio mkamilifu so nikaona kwa nini nisimsamehe, Harmonize nahaidi  nitakupenda leo kesho hadi milele”. amesema Kajala

About the author

mzalendoeditor