Featured Kitaifa

RC SINGIDA AKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA TASAF WILAYANI MKALAMA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Singa  Kata ya Kinampundu katika ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) aliyoifanya hivi karibuni wilayani Mkalama.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singa katika ziara hiyo.

Wananchi wakijiji cha Singa 
wakicheza ngoma wakati wakimkaribisha Mkuu wa wilaya katika ziara hiyo.

Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Mkalama  Lameck Itungi akizungumza katika 
ziara hiyo.

Wananchi wa kijiji cha Singa wakiwa kwenye mkutano wa mkuu
wa mkoa .

Katibu tawala wa Wilaya ya Mkalama,.Elizabeth Rwegasira
akifanya utambulisha kwa watumishi wa Halmashauri pamoja na msafara uliongozana
na Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Wataalamu
kutoka ngazi ya wilaya na Mkoa
wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa katika kijiji cha  Mnguli kitongoji cha Kipamba.

Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gumanga, James Mkwega akitoa neno la shukrani kwa serikali ya awamu ya sita  kwakutoa fedha za utekelezaji wa miradi kwa
wilaya ya Mkalama  ambapo pia
amesema  wataunga mkono juhudi za serikali
kwa kusimamia fedha 
za  miradi vizuri pamoja na kufanya kazi kwa
bidii kwa masilahi mapana ya wilaya na wananchi wa Mkalama.

Diwani wa Kata ya Mwangeza ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti
wa Halmshauri ya Wilaya ya Mkalama, Bosco Samwel akizungumza  kwenye ziara hiyo.

Wananchi wa Kijiji cha
Munguli Kitongoji cha Kipamba wakitumbuiza kwa ngoma za asili  za jamii ya Wahadzabe wakati wa ziara ya Mkuu
wa Mkoa katika  Kijiji  cha Munguli.

Mkutano
ukiendelea.

 Afisa Mazingira Wilaya ya Mkalama, Amon Sanga akieleza utekelezaji wa mradi wakurejesha
Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula unaotekelezwa katika Kata ya
Mpambala kwa vijiji vya Nyahaa, Mkiko, Mpambala , Lugongo pamoja na Kata ya
Mwangeza  Kijiji cha  Munguli.

Mratibu
wa TASAF Wilaya ya Mkalama, Gudluck Mlau akieleza namna mradi wa kunusuru
kaya masikini unavyotekelezwa
wilayani  humo.

Mratibu wa Sensa  Wilaya ya Mkalama, Daniel Tesha akieleza maandalizi ya sensa ya watu
na makazi  inayotarajiwa kufanyika Agosti
23 mwaka huu.

Mwenyekiti wa jamii ya Wahadzabe Edward Mashimba akitoa
neno la shukrani kwa ujio wa Mkuu wa Mkoa katika Kitongoji cha Kipamba ambapo
alisema jamii ya Wahadzabe iko tayari kushiki shughuli  zote zamaendeleo  pamoja na kushiriki katika zoezi la sensa ya
watu na makazi  ifikapo Agost 23 mwaka
huu.

  Mkuu wa Mkoa
wa  Singida Dkt. Mahenge akiwa katika
picha ya pamoja na wananchi wa jamii ya wahadzabe pamoja na wataalamu
mbalimbali wakati wa ziara hiyo.

Rachel Joram na Dotto Mwaibale,  Mkalama  

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt . Binilith mahenge ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutenga kiasi cha sh.2,118,079,899.00 kutoka  kwenye mfuko wa kimataifa wa mazingira katika
kutekeleza mradi  wa kurejesha Ardhi
iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula
katika kata ya Mpambala na Kata ya Mwangeza Kijiji cha Munguli Wilaya

ya  Mkalama mkoani Singida

Dkt. Mahenge aliyasema  hayo  katika
ziara aliyoifanya  wilayani hapa  ya kutembelea miradi  mbalimbali
ya maendeleo  inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF)  katika Kijiji cha  Singa Kata ya Kinampundu na  Kijiji cha Munguli Kitongoji cha Kipamba  Kata ya Mwangeza  na kusema  kukamilika kwa mradi hiyo itatatua changamoto

nyingi za wananchi ikiwani pamoja na
kutatua kero za maji, na kutunza mazingira , kuzuia  mmomonyoko  kwenye  maeneo

 yanayotekelezwa miradi.

Aidha amewataka wataalamu wa ngazi zote kusimamia vizuri
pamoja  kushirikiana kutatua  changamoto
zitakazojitokeza ili kuharakisha maendeleo ya  Wananchi wa wilaya ya mkalama ikiwa ni pamoja

na kutatua migogoro mbalimbali iliyopo katika maeneo  ya miradi.

Akitembelea bwawa la kijiji cha  Singa kata ya Kinampundu  liliochimbwa na wanufaika wa mradi wa kunusuru
kaya masikini TASAF aliwataka wananchi hao kutumia mradi huo vizuri ili uweze
kuwanufaisha kwakuwataka kulima kilimo cha umwagiliaji na kutoruhusu mifugo
kuingia na kukanyaga   kujaza mchanga  kwenye  mradi ili maji hayo yaweze kudumu  hadi kipindi cha masika.

Awali akimkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mkuu wa Wilaya ya Mkalama  Sophia  Kizigo alianza kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa

kutembelea wilaya ya mkalama  kujionea
maendeleo ya wilaya  na kuongeza kuwa  ziara yake inachochea kasi ya maendeleo kwani
wananchi wanajisikia furaha kutembelewa na viongozi wa kubwa huku akimuomba
Mkuu wa  mkoa Dkt . Mahenge inapotokea
kugawanywa maeneo ya utawala na Kata ya Mwangeza iangaliwe kwa jicho la pekee
kwani ni kubwa hivyo kupunguza ufanisi wa kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya
mbali.

Diwani wa Kata ya Mwangeza  Bosco  Samwel
aliongeza kuwa ni kweli Serikali imefanya mambo makubwa katika kata yake

na hasa kwa jamii ya Wahadzabe inayoishi
kijiji cha Munguli kitongoji cha Kipamba  lakini kilio
bado kipo kwenye ubovu wa miundo mbinu ya barabara , umeme, ukosefu

wa  nyumba za walimu pamoja na uhaba wawalimu
katika shule shikizi ya Kipamba ambayo tayari imesajiliwa pamoja na shule
shikizi ya Mwasulagi ambayo hakuna barabara ya kufika katika shule hiyo.

Afisa Mazingira Wilaya ya Mkalama  Amon Sanga alieleza
utekelezaji wa mradi wa mazingira umesaidia kuwepo kwa mpango wa matumizi bora
ya ardhi  kwa vijiji vitano
vinavyotekeleza mradi wa LDFS ,huku vikundi vya uzalishaji kiuchumi vikianza
kunufaika na ufugaji kwa kupata mizinga ya nyuki  420 pamoja na kuwepo kwa msitu ambao tayari
una hati miliki ya kimila unaotoa manufaa
mbalimbali  ikiwa ni pamoja na

ufugaji wa nyuki, upatikanaji wa mahitaji ya
jamii ya kihadzabe kama vile dawa,mizizi , matunda na wanyama pori.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa TASAF Mratibu wa TASAF Wilaya ya Mkalma, Gudluck Mlau alisema kuwa kwa kipindi cha Julai 2021 hadi
Mei  2022 Halmashauri ya Wilaya ya
Mkalama im epokea kiasi cha Tsh,.1,591,881,600.00 na malipo yamefanyika katika
vijiji vyote 70 ambapo jumla ya walengwa 7,235 walinufaika na mradi huo huku
kijiji cha Munguli kikipokea  fedha za
ruzuku  kiasi cha Tsh.43,998,000.00 kwa
kipindi cha mwezi  Januari  hadi Mei 2022 huku walengwa 354 wakipokea
ruzuku zao kwa njia ya mtandao jambo linalowapa urahisi  wakupokea fedha zao .

Sanjari na hayo  Mratibu
wa Sensa Wilaya ya Mkalama, Daniel Tesha
alieleza maandalizi ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika

Agosti 23 mwaka huu kuwa yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa  tayari
hamasa imeshafanyika kwa vijiji vyote70 vya wilaya ya Mkalama na tayari

eneo  Maalumu limetengwa katika kitongoji
cha Kipamba kijiji cha Munguli  maalumu
kwa jamii ya wahadzabe na bajeti maalumu
imewasilishwa ofisi ya Takwimu taifa
ili jamii hiyo iweze kupata chakula katika siku hiyo ya sensa na kuweza

kushiriki kikamilifu.

Baadhi ya wananchi wajamii ya wahadzabe wameishukuru
serikali kuweka kipaumbele na kupeleka miradi mingi katika jamii hiyo huku
wakiaahidi kuunga mkono  juhudi za
serikali kwa kufanya kazi kwa bidii na kushiriki zoezi la sensa  ya watu na makazi ifikapo Agosti 23 mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor