Uncategorized

MBUNGE CHIKOTA ATAKA MRADI WA UMWAGILIAJI KIJIJI CHA RUSHA CHINI KUTENGEWA FEDHA

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Jimbo la  Nanyamba (CCM),Abdallah Chikota ametaka mradi wa umwagiliaji wa Kijiji cha Arusha Chini utatengewa fedha ili uanze kutekelezwa.

Akiuliza swali leo Mei 26,2022 bungeni jijini Dodoma , Chikota amesema kuwa kuna eneo kubwa linazunguka Kijiji cha Ngonja, Arusha Chini na Arusha Juu na kuhoji serikali ipo tayari kujumuisha eneo hilo wakati wa kufanya usanifu wa skimu hiyo ya umwagiliaji.

Akijibu maswali hayo bungeni , Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, amesema  mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Arusha chini una hekta 120 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Amesema kuwa kati ya hizo hekta 48.5 zinamwagiliwa kwa kutumia mifereji ya asili ambayo chanzo chake cha maji ni chemichemi na mvua za msimu.

“Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa skimu hii,”amesema

Pia ameeleza kuwa  serikali ipo tayari kutoa maelekezo kwa timu itakayofanya usanifu kupitia eneo kubwa la skimu hiyo kadri iwezekanavyo.

“Maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeagiza ifikapo Mwaka 2025 eneo la umwagiliaji liwe Hekta Milioni 1.2, kwa hiyo wataalamu wataangalia eneo ambalo halijajumuishwa ili lijumuishe,”amesema

About the author

mzalendoeditor