Featured Kitaifa

MBOWE AANZA KAMPENI YA ‘JOIN THE CHAIN’ AKUSANYA PESA

Written by mzalendoeditor

MWEYEKITI  wa Chadema, Freeman Mbowe ameongoza matembezi ya mguu kwa mguu katika kata ya Kunduchi kwaajili ya kukusanya fedha za uendeshaji wa chama hicho.

 Machi 25, 2022 Makamu mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, akiwa Ubelgiji alizindua kampeni ya ‘Joing The Chain’ yenye lengo la kuchangia chama hicho kwaajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mkutano wa baraza kuu unaotarajiwa kufanyika Aprili 25 mwaka huu.

“Kampeni hii ni kwaajili ya kuchangia chama chochote ulichonacho, ili kufanya ukombozi wa kweli wa nchi yetu, dhuluma zimezidi gharama za maisha zimekuwa kubwa sana na kipato cha wananchi kimezidi kupungua,”alisema Mbowe.

About the author

mzalendoeditor