MWANAMITINDO, Msanii wa muziki na Bongo Movies Hamisa Mobeto,amesema  kuwa, huwa anachukizwa na baadhi ya watu kudharau kazi za watu wengine huku akisema kama ikitokea mtu akamfanyia hivyo wataishia kugombana.

Hamisa anasema kuwa, unaweza ukakuta mtu anakuita kwa ajili ya kwenda kufanya shoo ila ikifikia kwenye sehemu ya kutaja kiasi cha pesa, ukisema pesa kuwa tu hapo ujue ndiyo kwaheri huitwi tena.

“Hivi mtu unamuombaje msanii aje kufanya shoo, halafu akikupa bei yake unamjibu wasanii tunao wengi, vitu vingine bana, sasa si uwafuate hao wengi, huwa sipendezwi kabisa na mambo kama haya ndiyo maana mimi kwenye muziki nafanya kama kipaji wala sina muda wa kuhangaika na shoo maana najua kunilipa watanishindwa, tutaishia kugombana tu,” anasema Hamisa.

chanzo:Global 

Previous articleFIFA YATANGAZA MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA 2022 QATAR TIMU ZA AFRIKA ZAPANGWA NA VIGOGO
Next articleWANAFUNZI 238 WAHITIMU PROGRAMU MAALUMU CHUO CHA VETA SHINYANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here