Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji safi na salama baina ya RUWASA na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Ltd kwa ajili ya kufikisha huduma ya maji kwenye kata tatu za jimbo hilo

…………………………………………………

Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameshuhudia utiaji saini wa mkataba baina ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wa Mkoa wa Lindi na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Limited kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi na salama wa mradi wa Nnyangao – Mtama

Ujenzi wa mradi huo utanufainisha na kuwawezesha wananchi zaidi ya 22,000 kupata maji safi na salama ambao utagharimu zaidi ya shilingi 4,577,244,446

Mradi huo utatekelezwa jimboni humo kwenye kata tatu za Majengo, Mtama na Nyangao zenye jumla ya vijiji 13 vya Nyangao A, Nyangao B, Mtakuja II, Nangaka, Masasi, Majengo A, Majengo B, Mvuleni, Mihogoni, Mbalala, Makonde, Mnamba (Chluwe) na Mkwajuni

Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Nape ni Mhe. Shaibu Issa Ndemanga, Mkuu wa Wilaya Lindi; Mhe. Yusuph Abdalah Tipu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama; Waheshimiwa madiwani wa maeneo husika, watendaji wa Ruwasa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti comred Athumani Seif Hongonyoko.

Waziri Nape amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo

Previous articleAJALI:WATU SITA WAFARIKI DUNIA TANGA
Next articleROMAN ABRAMOVIC ADAI KUWEKEWA SUMU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here