Featured Kimataifa

ROMAN ABRAMOVIC ADAI KUWEKEWA SUMU

Written by mzalendoeditor

Bilionea wa Urusi Roman Abramovich anadaiwa kuwekewa sumu kwenye mazungumzo ya amani katika mpaka wa Ukraine na Belarus mapema mwezi huu, vyanzo vya karibu na bilionea huyo vimesema.

Mmiliki huyo wa Chelsea FC – ambaye kwa sasa amepona alikutwa na dalili zinazohusishwa na kuwekewa sumu na aliripotiwa kupata madhara kwenye macho na ngozi.

Wapatanishi wengine wawili wa amani katika mazungumzo ya Ukraine na Urusi wanasemekana pia wameathirika.

Chanzo cha karibu na Bw Abramovich kimeiambia BBC kuwa sasa amepona na anaendelea na mazungumzo ya kujaribu kumaliza vita nchini Ukraine.

CHANZO:BBCSWAHILI

About the author

mzalendoeditor