Kitaifa

WAZIRI MKENDA ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA “DOHA FORUM” JIJINI DOHA QATAR

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Pro.Adolf Mkenda akizungumza na Waziri wa Elimu wa Siera Leone David Moinina Sengeh mara baada ya Jukwaa la majadiliano juu ya uboreshaji Elimu jijini Doha, Qatar

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Viongozi kutoka UNICEF walipokutana katika Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo DOHA FORUM unaofanyika Jijini Doha, Qatar.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akiwa katika mazungumzo maalum na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Education Above All la Qatar Fahad Al- Sulaiti juu ya ushirikiano na Tanzania katika kuimarisha elimu Doha Qatar

Prof Adolf Mkenda Waziri wa Elimu Sayansi an Teknolojia akiwa katika Picha na Baadhi ya Mawaziri waluohudhururia Jukwaa la majadiliano ya kuleta mabadiliko sahihi katika Elimu ylililofanyika sambamba na Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Doha Forum,jijini Doha, Qatar

……………………………………………

Na.WyEST

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameshiriki Mkutano wa Kimataifa Doha Forum kuhusu masuala ya Maendeleo uliofanyika Machi 26 ,2022.

Mkutano huo unaofanyika kila Mwaka umeshirikisha viongozi na wataalamu kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo Mwaka huu umelenga katika kujadili jinsi ya kuleta mabadiliko chanya katika maendeleo.

Moja ya Agenda katika mjadala wa mkutano huo ni mabadiliko halisi na chanya katika elimu hususa baada ya athari za UVIKO 19 ambapo Waziri wa Elimu ameshiriki katika majadiliano hayo ambayo yanahusisha Mawaziri kutoka Nchi 9 ikiwemo Qatar ,Tanzania,Uganda, Sudan Kusini, Siera Leone na Somalia.

Akizungumza katika jukwaa hilo la majadiliano Prof. Mkenda amesema Tanzania kwa sasa iko katika hatua ya kufanya mapitio ya Sera na Mitala ili kuhakikisha Elimu inayotolewa inazingatia kujenga ujuzi na kwamba mpango huo ni shirikishi.

Nae Mtendaji Mkuu wa Shirika la Education Above all la Qatar Mhe. Fahad Al-Sulaiti amesema wakati umefika wa mataifa kuleta Mabadiliko sahihi katika Elimu kwa kuwa na Mitaala Sahihi, mbinu za kisasa za kufundishia, matumuzi ya TEHAMA katika kufundisha na ujifunzaji kulingana na mipango endelevu ya Nchi na kusisitiza juu ya suala la kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Elimu.

Wakati huo huo Waziri wa Elimu amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji huyo juu ya ushirikiano katika kuboresha Elimu Tanzania.

About the author

mzalendoeditor