Featured Kitaifa

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA,LSF NA UDOM WASAINI USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KUONGEZA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA NCHINI.

Written by Alex Sonna

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini  Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Shirika la Legal Service Facility (LSF),hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,MZALENDO BLOG-DODOMA

SERIKALI  imeendelea kuchukua hatua za kimkakati katika kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa haki nchini, baada ya Wizara ya Katiba na Sheria kuingia makubaliano mapya ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Shirika la Legal Services Facility (LSF), yenye lengo la kupanua huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.

Akizungumza  leo Januaria 8,2026 Mtumba jijini Dodoma wakati wa utiaji saini wa hati za ushirikiano baina ya pande hizo tatu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi,ameeleza  kuwa ni hatua muhimu katika mageuzi ya sekta ya haki, hususan kwa wananchi wa kipato cha chini na makundi maalumu yanayohitaji ulinzi zaidi wa kisheria.

Bw.Maswi amesema kuwa utiaji saini huo si tukio la kawaida, bali ni hatua yenye uzito wa kisera, kikatiba na kiutendaji inayolenga kuondoa vikwazo vya kimfumo vinavyowakwamisha wananchi kupata haki kwa wakati.

“Haki si anasa wala zawadi. Ni msingi wa amani, mshikamano wa kitaifa na maendeleo ya taifa. Makubaliano haya ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki bila ubaguzi—bila kujali hali ya kiuchumi au kijiografia,” amesema Bw.Maswi

Aidha, amelitaja  Shirika la LSF kama mdau wa kihistoria na wa kimkakati, ambaye ameendelea kuisaidia Serikali hata kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria.

Maswi amesema LSF imekuwa na mchango mkubwa katika kujenga uwezo wa Wasaidizi wa Kisheria nchini, na kupitia makubaliano hayo, uwekezaji utaongezwa kwenye mafunzo endelevu, vitendea kazi, TEHAMA, miundombinu ya ofisi na usafiri ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa ufanisi na kwa viwango vinavyokubalika.

“Huu ni ushahidi kwamba mashirikiano ya kweli kati ya Serikali na wadau yanaweza kuleta mabadiliko ya kudumu na yenye tija kwa wananchi,” amesisitiza.

Hata hivyo amesema kuwa kupitia makubaliano kati ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma, wamekubaliana kushirikiana katika maeneo ya msingi na ya kimkakati.

Amesema  makubaliano hayo yamejikita katika maeneo ya kimkakati na ya msingi, ikiwemo utoaji wa elimu ya kisheria kwa wananchi, kufanya tafiti kuhusu upatikanaji wa haki, pamoja na kuanzisha na kuendesha Kituo cha Pamoja cha Msaada wa Kisheria katika ngazi ya mkoa.

Bw.Maswi amesema kuwa kituo hicho kitakuwa nguzo muhimu katika utoaji wa huduma jumuishi, kikitoa uwakilishi wa kisheria kwa wananchi wasioweza kumudu gharama za mawakili binafsi, sambamba na kuwa kituo cha rufaa kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.

“Huu ni mfano halisi wa utekelezaji wa sera kwa vitendo—sera inayoshuka kutoka kwenye maandiko kwenda moja kwa moja kwa mwananchi,” amesema Bw.Maswi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility (LSF) Bi.Lulu Ng’wanakilala,amesema  upatikanaji wa haki ni haki ya kikatiba na msingi wa utawala bora, akibainisha kuwa bila mifumo imara ya msaada wa kisheria, haki hiyo hubaki kuwa ndoto kwa wananchi wengi.

“Kwa mwaka huu, ajenda ya uendelevu wa huduma za msaada wa kisheria ndiyo kipaumbele chetu. Kupitia MoU hii tunathibitisha dhamira ya kuunga mkono jitihada za Wizara katika elimu ya sheria kwa umma, tafiti, mijadala ya kitaifa na uhamasishaji wa rasilimali,” amesema Bi.Lulu

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi), Prof. Razack Lokina, amesema  ushirikiano huo unaimarisha nafasi ya UDOM kama mshirika wa kimkakati wa Serikali katika kukuza haki na utawala bora.

Prof.Lokina amesema  makubaliano hayo yatapanua wigo wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi, hususan makundi maalumu kama wanawake, watoto, wazee, watu wenye ulemavu na wananchi wasio na uwezo wa kifedha, sambamba na kuongeza uelewa wa Katiba na Sheria katika jamii.

“Ushirikiano huu utaimarisha umahiri wa vitendo kwa wanafunzi wetu wa sheria, hivyo kuzalisha wanasheria mahiri, waadilifu na wenye mtazamo wa kuhudumia jamii tangu wakiwa vyuoni. Hii itasaidia kuongeza ufanisi wa utawala wa sheria nchini na kupunguza msongamano wa kesi katika vyombo vya utoaji haki,” amesisitiza.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility (LSF) Bi.Lulu Ng’wanakilala,wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano  baina ya Wizara ya Katiba na Shirika la Legal Service Facility (LSF) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Bi.Lulu Ng’wanakilala,wakibadilisha  hati za makubaliano ya ushirikiano  baina ya Wizara ya Katiba na Shirika la Legal Service Facility (LSF) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mara baada ya kusaini Mkataba huo,hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Bi.Lulu Ng’wanakilala,wakionyesha  hati za makubaliano ya ushirikiano  baina ya Wizara ya Katiba na Shirika la Legal Service Facility (LSF) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mara baada ya kusaini Mkataba huo,hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi (kushoto) akiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi), Prof. Razack Lokina,wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano  baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na  Shirika la Legal Service Facility (LSF)  hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi (kushoto)  akiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi), Prof. Razack Lokina, wakibadilishana  hati za makubaliano ya ushirikiano  baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na  Shirika la Legal Service Facility (LSF) hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi,akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Shirika la Legal Service Facility (LSF),hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility (LSF) Bi.Lulu Ng’wanakilala,akitoa salamu wakati wa hafla ya kutia saini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Shirika la Legal Service Facility (LSF) pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ,hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi), Prof. Razack Lokina,akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Shirika la Legal Service Facility (LSF),hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

 

SEHEMU ya Washiriki wakifuatilia  hafla ya kutia saini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Shirika la Legal Service Facility (LSF),hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini  Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Shirika la Legal Service Facility (LSF),hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini  Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Shirika la Legal Service Facility (LSF),hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu,Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini  Hati za Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Wizara ya Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Shirika la Legal Service Facility (LSF),hafla iliyofanyika leo Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma.

About the author

Alex Sonna