Uncategorized

MTAFITI AISHAURI SERIKALI HATUA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Written by mzalendoeditor


MTAFITI Mwandamizi kutoka Taasisi inayojihusisha na Tafiti katika Nyanja za Uchumi na Jamii (ESRF) Vivian Kazi akizungumza wakati wa kikao hichoMtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) Morogoro Dk Winifred Mbungu akizungumza


Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia kwa umakini

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia kwa umakini 

NA OSCAR ASSENGA,TANGA
MTAFITI
Mwandamizi kutoka Taasisi inayojihusisha na Tafiti katika Nyanja za
Uchumi na Jamii (ESRF) Vivian Kazi ameishauri Serikali kuona namna nzuri
ya kuweza kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa
kuhakikisha wakulima wanalima kilimo kinachostahimili ukame
Vivian
aliyasema hayo wakati wa kikao chao cha kuwasilisha utafiti ambao
ulifanywa na Taasisi hiyo na Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro (SUA) kwa
awamu mbili mwaka 2019 na 2021 lengo kubwa wamechagua Tanga kama eneo
lenye sifa ya hali ya hewa inayowakilisha maeneo mengi nchini hali ya
hewa nzuri kwenye nyanda za juu na chini   
Vivian
ambaye pia ni  Mkuu wa Idara inayojihusisha na tafiti za kimkakati na
machapisho na ESFR kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Leeds,Abadin vya
Uingereza,Sua na Chuo cha Ku cha Nelson Mandara Arusha wamekuwa
wakifanya kazi ya mradi unaojihusisha na mabadiliko ya Tabia ya nchi.
Mradi
huo wa miaka minne umefanyika na mapendekezo waliyoyatoa ni kuweza
kulima kilimo stahimilivu na mabadiliko ya tabia ya nchi kuweza kutumia
teknolojia ya chini au kati ili kuongeza kilimo tija na kuweza kulima
mazao ambayo yataweza kustahimili mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumzia
athari za mabadililo ya nchi,Vivian alisema mabadiliko ya tabia ya nchi
yameathiri nchi nyingi tajiri na masiki ikiwemo kuathiri kwa kiasi
kikubwa mabadilko ya mvua hatua ambayo inasababisha mazao kutokuua kwa
wingi wakati wa mavuno.
 “Kwenye
tafiti zenu tuliliona hilo na ifikapo mwaka 2050 kama zisipochukuliwa
juhudi za makusudi athari zitakuwa kubwa kiasi huku wakishauri hatua
zianze kuchukuliwa mapema kuweza kukabiliana nazo”Alisema
Alisema
lengo la mkoa wa Tanga kuwepo miongoni mwa mikoa kwenye mradi huo
unaojihusisha na mabadiliko ya tabia ya nchi kilimo stamilivu na usalama
wa chakula kwa Tanzania kutokana na kuwa eneo lenye sifa ya hali ya
hewa inayoweza kuwakilisha maeneo mengi nchini na kuna mpango wa
kuongeza uwezo maafisa kilimo,maafisa ugavi.
Aidha
alisema mradi huo ambao ulianza mwaka 2018 ambao ni wa miaka minne una
lengo la mradi kushauri kwenye mambo ya sera kitu gani kifanyike kwa
Tanzania kuhakikisha wanapambana na mabadiliko hayo ya tabia ya nchi.
Aliongeza
namna ya kukabiliana nao ni kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya
nchi kwa wakulima kulima kilimo stamilivu na kuangalia mazao
yanayostahimili mabadilio hayo pamoja na usalama wa chakul,lishe na
biashara kama watapata satras.
“Lakini
kuna mafanikio mengi kwenye mradi mpango wa kuongeza uwezo maafisa
kilimo,maafisa ugavi ,watafiti na wamefanya tafiti kwenye sera kwa
kuhojiana na wadau mbalimbali  katika ngazi za wizara na ngazi za idara
serikali na wakala mbalimbali”Alisema  
Hata
hivyo aliwataka maafisa ugani mkoani Tanga kutumia vema elimu waliopewa
 na taasisi hiyo ili kuweza kuwasaidia wakulima kuweza kulima kwa tija
na kuondokana na kulima kimazoea ambapo wakati mwengine wanakosa mavuno.
Vivian
aliyasema hayo wakati walikuwa na mkutano wao na watafiti na maafisa
kilimo kutoka wilaya ya Muheza na Lushoto zilizopo mkoani Tanga kuweza
kuwasilisha utafiti ambao
Awali
akizungumza wakati wa mkutano huo Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo
(SUA) Morogoro Dk Winifred Mbungu  alisema ameshiriki kwenye utafiti na
watalamu mwengine kutoka nchi za Afrika ambazo ni Malawi ,Zambia,Afrika
Kusini na Tanzania  yeye pamoja na wengine wameshiriki kujaribu kuona
mkusanyiko kufanya utafiti kwa ajili ya kuangalia athari diet na gesi.
Alisema
katika utafiti huo ulikuwa shirikishi wao kama nchi walikwa wanaangalia
wanapokwenda na kuangalia namna gani wanaweza kustahimili mabadiliko
walilenga miaka 2050 ambapo mabadiliko yanatokea na maendelea
yanatokokea.
Alisema
miaka 2050 inakadiriwa joto linatarajiwa kuongezeka na linakwenda
kuathiri mazao hasa ya wanayozalishwa lakini zao hilimilivu ni soya
ambalo linaweza kuthimili na kwa Tanzania wana watu wanaokadiriwa
milioni 60 na kwa mwaka 2050 inakadiriwa kutakuwa na watu milioni 100
sasa wanatakiwa wawe wanazalisha chakula ardhi hiyo hiyo hawataweza
kwenda mbele kama hawatutaingiza teknolojia.
Kwa
upande wake Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Emigidius Kasunzu
aliwataka maofisa kilimo kutumia elimu waliyoipata kuwaelekeza wakulima
kulima mazao yanayohimili hali ya ukame .
Aliwataka
wataalamu wa kilimo na waatafiti kufanya utafiti na ugunduzi wa mbegu
bora pamoja na tekinolojia ya kisasa ili wakulima waweze kuwasaidia
 kulima kulima kilimo chenye tija. 

Uvunaji wa maji utunzaji wa mazinhira pamoja na upatikanaji wa mbegu
bora utaweza kutusaidtia kujiepusha na baa la njaa kwa siku za mbeleni ‘
Amebainisha Kasunzu

 

About the author

mzalendoeditor