Featured Michezo

MACEDONIA YAISHANGAZA DUNIA,YAIONDOA ITALIA KOMBE LA DUNIA 2022

Written by mzalendoeditor

Huzuni kwa wataliano Mabingwa wa Ulaya Italia kwa mara ya pili hawatacheza  tena Kombe la Dunia la 2022 baada ya kufanyiwa unyama wa aina yake kutoka kwa Macedonia ya Kaskazini kwa kichapo cha bao 1-0 na kutupwa nje katika mechi yao ya mchujo mjini Palermo.

Aleksandar Trajkovski alitegema pasi iliyolegea katika dakika ya 92, akasonga mbele na kuachia bao la ushindi kutoka nje ya eneo la hatari.

Bao hilo liliibua shangwe kali kwenye benchi ya Macedonia Kaskazini, huku wachezaji wa Italia na wakufunzi wakipiga magoti mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.

Italia inashindwa kufuzu kombe la Dunia 2022 kwa mara nyingine tena baada ya kukosa kombe la Dunia la 2018.

Ni miezi minane tu tangu kikosi cha Roberto Mancini kusherehekea moja ya ushindi wao mkubwa zaidi – kwa kuwashinda Uingereza katika uwanja wa Wembley na kushinda Euro 2020 baada ya kuchukuliwa kuwa wachezaji wa nje watakaoshiriki dimba hilo.

About the author

mzalendoeditor