Uncategorized

WAZIRI GWAJIMA ATAKA KASI UANZISHWAJI WA MADAWATI YA JINSIA KWENYE VYUO VYA ELIMU YA JUU NA KATI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima ,akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati akifungua baraza hilo lililofanyika leo  Machi 23,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima ,akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati akifungua baraza hilo lililofanyika leo  Machi 23,2022 jijini Dodoma.

MWENYEKITI  wa Baraza la Wafanyakazi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amabye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula,akielezea mikakati ya baraza kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza hilo lililofanyika leo  Machi 23,2022 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Ikusubisya Kasebele akiwasilisha mada kwa niaba ya watumishi wa Wizara hiyo katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika leo Machi 23,2022 jijini Dodoma.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakifuatilia matukio katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika leo Machi 23,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo mara baada ya kuzindua baraza hilo lililofanyika leo  Machi 23,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima ,akiagana na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua baraza hilo lililofanyika leo  Machi 23,2022 jijini Dodoma.

……………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametaka kuongezeka kasi katika uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu na kati.

Hayo ameyasema leo Machi 23,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa baraza la Wafanyakazi lililowakutanisha kwa ajili ya kujadili masuala ya wafanyakazi na kupitia mpango wa Bajeti kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

DK. Gwajima  amesema kuwa Wizara iliandaa mwongozo na kuratibu uanzishwaji wa madawati haya kwa lengo la kuweka mfumo wa kushughulikia masuala ya unyanyasaji wa kingono na vitendo vya ukatili katika vyuo vya elimu ya juu na kati na kuimarisha ulinzi wa wanawake na watoto dhidi ya vitendo hivyo.

“Katika vyuo hivi nimefuatilia takwimu, kasi ya uanzishwaji wa madawati haya ni ndogo sana, hivi vyuo vilitakiwa vione umuhimu wa uwepo wa madawati haya, nadhani kuwe na mawasiliano kati ya Baraza hili na mabaraza ya vyuo kuona sera ya usawa wa kijinsia katika vyuo inavyotekelezwa” ameeleza Dkt. Gwajima.

Aidha Dk.Gwajima ameoneshwa kusikitishwa na baadhi ya wafanyakazi wa vyuo kuwa vikwazo vya uanzishwaji wa madawati hayo kwa wao wenyewe kufanya unyanyasaji wa kijinsia.

Hata hivyo amesema kuwa Serikali itahakikisha mwongozo huo unafika hadi katika shule za Msingi na Sekondari ili kusaidia mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.

‘Dunia yote kwa sasa inaelekea kwenye kuimarisha usawa wa kijinsia hasa kwenye masuala ya kiuchumi hivyo ametoa wito watanzania kujipanga kupata fursa hizo kupitia Kamati iliyoundwa kuratibu utekelezaji wa ahadi za nchi katika jukwaa la usawa wa kijinsia.”amesisitiza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Zainab Chaula, amesema kuwa Wizara itaendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ili kutokomeza vitendo vya ukatili kwani ndiyo msingi katika kuimarisha usawa wa kijinsia.

“Suala la ukatili wa kijinsia tumelishikia bango japo bado halijaongelewa vya kutosha, tutaendelea kwa kushirikiana na wadau. Vilevile kuhakikisha tunatatua changamoto ya uhaba wa watumishi, ukosefu wa ajira na uchakavu wa majengo hasa ya makazi ya wazee” amesema Dkt. Chaula.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE katika Wizara hiyo Ikusubisya Kasebele amesema kuwa Baraza hilo litafuata sheria pamoja na kukaa kikao mara mbili kwa mwaka na kuhusisha wajumbe kutoka maeneo yote yanayosimamiwa na Wizara hiyo.

Aidha Kasebele amesema kuwa wajumbe wote wana haki ya kuchangia mawazo yao ikiwemo kupitia bajeti iliyoandaliwa kwa maslahi ya Taifa.

About the author

mzalendoeditor