Uncategorized

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA ARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA RAIS SAMIA.

Written by mzalendoeditor

Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, David Concar akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Mwanza 

Mwenyeki wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza  Edwini Soko (kushoto) akizungumza wakati wa  kumkaribisha Balozi David Concar kuzungumza na waandishi wa habari 

Balozi David Concar (Katika) akiwa na wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika picha ya pamoja 

………………………………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza

Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania David Concar amesema wanaridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari leo hii Ijumatatu Machi 21,2022 kabla ya kuanza ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Uingereza.

Amesema kuwa Rais Samia amekuwa akifanya teuzi mbalimbali za uongozi kwa usawa ambapo hali hiyo imesaidia masuala ya kisiasa kuzidi kuboreshwa zaidi.

Amesema kuwa mahusiano mazuri anayoyajenga Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu na Nchi mbalimbali ni mahusiano yenye tija kwa uchumi imara wa Taifa na mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza ( MPC), Edwini Soko amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania vyombo mbalimbali vya habari vimeimerika kwa kuwa na uhuru wa kuripoti maudhui mbalimbali yenye tija kwa Jamii.

About the author

mzalendoeditor