Featured Kitaifa

RAIS SAMIA APOKEA TAARIFA YA KIKOSI KAZI CHA KURATIBU MAONI YA WADAU WA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe wa Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa mara baada ya kupokea Taarifa yao Ikulu Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe wa Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa mara baada ya kupokea Taarifa yao Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao mara baada ya kupokea Taarifa yao Ikulu Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa mara baada ya kupokea Taarifa yao Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Machi, 2022.

 PICHA NA IKULU

.………………………………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vyama vya siasa kuzingatia usawa wa kijinsia kwa kutoa nafasi kwa wanawake ili waweze kushiriki katika siasa ndani ya vyama vyao.  

 

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akipokea taarifa ya Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

Aidha, Rais Samia amewataka wanawake kujua wajibu wao katika vyama vyao na katika jamii kwa ujumla na kuhakikisha kuwa wanaelewa ipasavyo ajenda zinazowasemea wanawake.  

 

Rais Samia amekitaka kikosi kazi hicho kuchambua masuala yote ambayo hayaleti siasa zenye tija, kukwaza demokrasia na kufanya siasa kuwa za chuki. 

 

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameeleza kuwa ipo haja ya kuwa na Kanuni za maadili za vyama vya siasa kitaifa (general codes of conducts) na kukiagiza kikosi kazi hicho pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa kuzipitia na kuimarisha Kanuni zilizopo ili zilete tija na zisiwe kandamizi.  

 

Vile vile Rais Samia ametoa rai kwa vyombo vya habari kuwa na uhusiano chanya na vyama vya siasa bila kuwa na upendeleo baina ya Serikali na vyama vya siasa. 

 

Kikozi kazi hicho kimeandaa mpango kazi kwa kuzingatia mambo kadhaa ikiwemo mchakato wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ambapo masuala ya muda mfupi yatakamilishwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu Kikosi Kazi kuanza.  

Vile vile, masuala ya muda wa kati yatafanyiwa kazi na kukamilika tangu sasa na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 huku masuala ya muda mrefu yatafanyiwa kazi baada ya Uchaguzi huo ikiwemo mchakato wa Katiba Mpya.  

About the author

mzalendoeditor