Featured Kitaifa

DKT. YONAZI ALIKUMBUSHA JESHI LA POLISI WAJIBU WA KUJIFUNZA NA KUTOA ELIMU YA USALAMA MTANDAO

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi,akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo Machi 21,2022, jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi,akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo Machi 21,2022, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) CP Camilius Wambura  akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo Machi 21, 2022, jijini Dodoma.

Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, (DCP) Ally Lugendo akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo  Machi 21, 2022, jijini Dodoma.

Mkaribu Mwandamizi wa Polisi, (SSP) Joshua Mwangasa akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi yaliyofanyika leo  Machi 21,2022, jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Usalama Mtandao kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, wakifatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Usalama Mtandao iliyotolewa na Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (hayupo pichani) yaliyofanyika leo  Machi 21,2022, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) CP Camilius Wambura  (wa pili kushoto), Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, (DCP) Ally Lugendo ( wa kwanza kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Usalama Mtandao kutoka Jeshi la Polisi baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo, jijini Dodoma.

…………………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi, amefungua mafunzo ya makosa ya mtandao (Cybercrime) huku  akiwataka  Wakuu wa upelelezi Mikoa  kuhakikisha wanawalinda wananchi  katika masuala ya uhalifu wa kimtandao.

Akifungua mafunzo hayo leo Machi 21 Jijini Dodoma,Dk.Yonazi amewataka wakuu hao kutumia mafunzo hayo katika kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao kwa kujifunza zadi kuhusiana na masuala hayo ili wawe wabobezi.

Walioshiriki mafunzo hayo ni Askari 100 kutoka Jeshi la Polisi wakiwemo Wakuu wa Upelelezi  Mikoa, pamoja na vikosi,wakuu wa madawati ya  upelelezi wa Makosa ya  mtandao wa Mikoa na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Polisi.

DK.Yonazi ,amewataka  Wakuu hao wa upelelezi kuhakikisha wanawalinda wananchi wote kwaajili ya usalama wao na mali zao kwa maslahi mapana ya Taifa.

“Nimefurahi tumekuja kujifunza jambo muhimu,tuliopo hapa tumekuja kupata elimu kwa wataalamu halisi dunia yetu inabadilika  sana mfano sasa hivi ugomvi wa Urusi na Ukraine  na mnafahamu pamoja na vita lakini ipo vita ya kidigital na uhalifu sio wa ndani pekee.Unaweza ukatendwa kwa kukusudiwa au kwa  kutokukusudiwa,”amesema.

Amesema mafunzo hayo  ni muhimu kwani yanawaonesha  nini tunatakiwa kufanya katika usalama wa Nchi  na raia

“Ni muhimu tukitoka hapa ukumbuke una wajibu wa kujifunza kila siku, mafunzo haya ni muhimu sana yameelekezwa kutoonesha njia ya nini tunatakiwa kufanya ili kuhakikisha usalama wa raia unakuwa timamu,”amesema

“Wizara inayowajibu kuhakikisha usalama unazingatiwa ipasavyo ndio maana tumeleta haya mafunzo na niendelevu kwa sababu teknolojia inabadilika. Mawasiliano yanazidi kuwa ya haraka kitu muhimu ni jinsi ya kuhifadhi taarifa,”amesema.

Naye,Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya  jinai nchini (DCI),Kamishna Camilius Wambura,amesema mafunzo hayo yanahusisha washiriki 100 kutoka Jeshi la Polisi wakiwemo Wakuu wa Upelelezi  Mikoa, pamoja na vikosi,wakuu wa madawati ya  upelelezi wa Makosa ya  mtandao wa Mikoa na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Polisi.

Amesema mafunzo hayo yatakuwa ni chachu kwa Jeshi la Polisi na malengo ni kila Askari awe na elimu kuhusu makosa ya mtandao ambayo kwa sasa yameshika kasi.

“Baada ya watendaji wa chini kupata mafunzo sasa tumeona ni zamu ya watendaji hawa na yamefadhiliwa na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.Tunatoa shukrani kwa Wizara kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa askari wetu,”amesema.

Amesema teknolojia inabadilika bila kushikana mkono hawawezi  kufikia lengo hasa katika makosa ya mtandao.

“Jeshi la Polisi tunahusika kukabiliana na makosa ya mtandao hivyo tunayachukulia kwa umuhimu mafunzo haya niombe mafunzo kama haya yaendelee kuwepo kwetu,naamini na washiriki wanalichukulia kwa umuhimu jambo hili,”amesema.

 

About the author

mzalendoeditor