Featured Kimataifa

BREAKING NEWS:SPIKA WA BUNGE LA UGANDA AFARIKI DUNIA

Written by mzalendoeditor

latest03pix

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kifo cha Spika wa Bunge la 11 la Uganda, Jacob Oulanyah.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Museven amesema kuwa Oulanyah amefariki leo Jumapili Machi 20, 2022 nchini Marekani ambako alikuwa akitibiwa.

Katika salamu zake za rambirambi, Museveni alisema Oulanyah ni Kada mzuri, na kwamba alilazimika kuchelewesha tangazo hilo ili watoto wake wapate taarifa kwanza.

“Nilipata taarifa za habari hizi za kusikitisha saa 10:30 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki kutoka kwa Watu ambao wamekuwa naye pamoja na daktari aliyekuwa akimhudumia katika chumba cha wagonjwa mahututi,” Amesema Rais Museveni

Jacob Oulanyah, ambaye mara ya mwisho alionekana Bungeni mnamo Desemba 2021, alikaa kwa wiki kadhaa huko Seattle, USA ambapo alikuwa akipokea matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari wake.

Mwanasiasa huyo ambaye maefariki akiwa na umri wa miaka 56 alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu mnamo Februari 4 baada ya kukaa kwa wiki katika Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa ya Mulago.

Marehemu Oulanyah alichaguliwa kushika nafasi ya Spika mnamo Mei 24, 2021 baada ya kumshinda aliyekuwa Spika Rebecca Alitwala KadagaAliwahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Uganda, kuanzia Mei 2011 hadi Mei 2021.

Oulanyah pia alikuwa mbunge anayewakilisha Eneobunge la Kaunti ya Omoro, Wilaya ya Omoro, eneo dogo la Acholi, katika Mkoa wa Kaskazini mwa Uganda.

About the author

mzalendoeditor