Featured Kimataifa

AKAMATWA KWA ‘KUMFANYIA’ BABA YAKE MTIHANI WA KITAIFA

Written by mzalendoeditor

Maafisa wa polisi katika mji wa Busia Magharibi mwa Kenya wanamzuilia kijana wa miaka 26 aliyekamtwa akijaribu kumfanyia baba yake (mtahiniwa wa kibinafsi) mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE).

Kwa mujibu wa ripoti za Gazeti la Daily Nation, polisi walifahamishwa na msimamizi wa mitihani wa kituo kimoja kwamba wanashuku kuna mtu anayejifanya kuwa mtahiniwa kwa lengo la kufanya mtihani kwa niaba ya mtahiniwa halisi.

Baada ya kupokea taarifa maafisa wa usalama walifika shuleni hapo mara moja.

“Tulipomhoji mshukiwa alikiri kutumwa na mtahiniwa kwa jina Josephat Basoga Makokha ambaye pia ni baba mzazi wa mshukiwa,” alisema Naibu Kamishena Mkuu wa jimbo la Busia.

Ripoti zaidi zinadai kuwa Bw. Barasa alitumia njia ya udanganyifu kuingia chumba cha mtihani kabla ya njama yake kutibuka.

About the author

mzalendoeditor