Featured Kitaifa

MTOTO MIAKA 14 AHUKUMIWA KIFUNGO KWA KOSA LA KUBAKA WILAYANI LUDEWA

Written by mzalendoeditor

Mahakama ya Watoto wilayani Ludewa mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha nje cha miezi 4 mtoto mwenye umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) mkazi wa kijiji cha Shaurimoyo wilayani humo ambaye ni mhitimu wa darasa la saba kwa kosa la kumbaka mtoto (jina lake limehifadhiwa)mwenye umri wa miaka 9 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza.

Hukumu hiyo imetolewa March 14, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo Isaac Ayengo baada ya mtuhumiwa huyo kukiri kutenda kosa hilo.

Aidha Amesema kifungo hicho kitaambatana na kumlipa faini ya shilingi 400,000 muhanga wa tukio hilo kwa kipindi cha miezi minne, mtuhumiwa kuripoti kwa Afisa ustawi wa jamii mara moja kwa wiki kwa kipindi cha miezi minne, mtuhumiwa kutii maelekezo ya Afisa ustawi wa jamii, Mtuhumiwa kuhudhuria shuleni kwaajili ya kuanza kidato cha kwanza, mtuhumiwa kutoingia katika maeneo ya burudani/starehe.

Awali akisomewa shitaka hilo na Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo Asifiwe Asigile mtuhumiwa huyo alidaiwa kuwa mnamo Januari 31, 2022 katika kijiji cha Shaurimoyo majira ya jioni mtoto huyo alitenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha 130(1)(2)e na 131(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya16 marejeo 2019.

Aliendelea kwa kusema kuwa mtuhumiwa huyo alikiri kutenda kosa hilo pamoja na hoja 9 za upande wa Jamhuri na kupelekea kupokea ripoti ya Afisa Ustawi wa jamii iliyohusu makuzi na maisha ya mtuhumiwa huyo huku katika maombolezo yake akisema kuwa ni mara yake ya kwanza hivyo anaomba asamehewe.

About the author

mzalendoeditor