Featured Kitaifa

DC MBONEKO AKAGUA MIRADI MAJI INAYOTEKELEZWA NA RUWASA SHINYANGA MAADHIMISHO WIKI YA MAJI

Written by mzalendoeditor
 

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akifungua Maji Bombani katika kituo cha kuchotea maji kwenye shule ya msingi Masengwa wilayani Shinyanga, (katikati) ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela na (wapili kutoka kulia) ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambayo inatekelezwa na wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilayani humo.

 

 

Mboneko amefanya ziara hiyo leo March 16,2022, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani, ambacho kilele chake ni Machi 22 mwaka huu, na alikuwa ameambatana viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na chama cha mapinduzi CCM wilayani humo.
Alisema katika miradi ya maji ambayo ameitembelea, amekuta imeshakamilika kwa asilimia kubwa, na kuanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

 

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi, na leo nimeona kazi ambayo imefanyika ambapo miradi inataoa maji, na katika maadhimisho ya wiki ya maji hapa Shinyanga sisi ni kufungulia maji kwenye mabomba tu na kumtua ndoo kichwani mwanamke, na kumuondolea adha ya kufuata maji umbali mrefu,” alisema Mboneko.

“Katika miradi hii ya maji ambayo imetekelezwa na wasihi wananchi muitunze miundombinu yake na kutoiharibu, ili idumu kwa muda mrefu kuwa hudumia na kuendelea kupata maji safi na salama,” aliongeza.

Aidha, alizionya kamati za maji kuwa pesa ambazo watakuwa wakizikusanya kwenye vituo vya kuchotea maji, wazipeleke benki kwenye akaunti husika na siyo kuzifanyia ubadhilifu.
Pia, aliwataka watu ambao wanasimamia kuuza maji kwenye vituo, wawepo muda wote na siyo kuanza kutafutwa, ili wananchi wafurahie huduma hiyo ya maji safi na salama na kuacha kutumia maji yasiyofaa.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela, amepongeza utekelezaji wa miradi hiyo ya maji, na kubainisha kuwa huo ndiyo utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa vitendo.
Nao baadhi ya akina mama akiwamo Rebeka Mpuya na Jesca Masanja, walisema huduma hiyo ya maji kuwa karibu, imewaondolea changamoto ya kufuata maji umbali mrefu, na hawataugua tena magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Maji vijijni (RUWASA) wilayani Shinyanga Emmael Nkopi, alisema asilimia kubwa ya miradi ya maji ambayo wanaitekeleza wilayani humo umeshakamilika, na mingine kuanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa maji safi na salama katika Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga, na kupongeza kazi kubwa ambayo wanaifanya Ruwasa ya utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo.Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela, akizungumza kwenye ziara hiyo ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo.
Diwani wa Masengwa Nicodemas Simon, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani.
Diwani wa Iselamagazi Isack Sengerema, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani.
Diwani wa Salawe Joseph Buyugu, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani.
Mwanafunzi Betha Emmanuel ambaye anasma shule ya msingi Masengwa, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA)wilayani Shinyanga, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani, ambapo shule hiyo nayo ni wanufaika wakuu wa mradi wa maji safi na salama shuleni hapo.
Mwanamke Ester Jilala mkazi wa kijiji cha Ibubu Kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga akielezea furaha ya kupata maji safi na salama kijijini humo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la LifeWater International, Devocatus Kamara akiwa katika Gati la maji kijiji cha Mishepo akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) kuhusu Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira katika vijiji vya Bushoma na Mishepo kata ya Mwantini halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akinawa mikono kwenye Kituo cha Kunawia mikono katika shule ya Msingi Bushoma kata ya Mwantini kilichojengwa na Shirika la LifeWater International. Vituo vingine vimejengwa katika shule ya Msingi Jimondoli na Ng’hama katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la LifeWater International, Devocatus Kamara (katikati) akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kuhusu Kituo cha kunawia mikono katika shule ya Msingi Bushoma kata ya Mwantini kilichojengwa na Shirika la LifeWater International kwa kushirikiana na Ruwasa.
Wanafunzi wakinawa mikono kwenye kituo cha kunawia mikono katika shule ya Msingi Bushoma kata ya Mwantini kilichojengwa na Shirika la LifeWater International kwa kushirikiana na Ruwasa
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiangalia Wanafunzi wakinawa mikono kwenye kituo cha kunawia mikono katika shule ya Msingi Bushoma kata ya Mwantini kilichojengwa na Shirika la LifeWater International.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akifungua Maji Bombani katika kituo cha kuchotea maji kwenye shule ya msingi Masengwa wilayani Shinyanga, (katikati) ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela na (wapili kutoka kulia) ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (katikati) akifungua Maji Bombani katika kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Ibubu Kaya ya Iselamagazi wilayani Shinyanga, (kulia)ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela na (kushoto) ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akifungua Maji Bombani katika kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Buduhe kilichopo Kata ya Salawe wilayani Shinyanga, (katikati) ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela na (kushoto) ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akimtwisha ndoo ya maji mwanamke Mary Station mkazi wa kijiji cha Buduhe Kata ya Salawe wilayani Shinyanga, alipofika kuona mradi wa maji katika kijiji hicho.
Wananchi wakishuhudia ufunguaji wa maji bombani kwenye vituo vya kuchotea maji, katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko alipotembelea miradi ya maji wilayani Shinyanga, katika maadhimisho ya wiki ya maji duniani.
Wananchi wakiendelea kushuhudia ufunguaji wa maji kwenye vituo vya kuchotea maji, katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko alipotembelea miradi ya maji wilayani Shinyanga, katika maadhimisho ya wiki ya maji duniani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (katikati) akiwa katika Ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji wilayani Shinyanga ambayo inatekelezwa na wakala wa maji vijijini (RUWASA).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati) akipiga picha ya pamoja na watumishi wa RUWASA wilayani Shinyanga, mara baada ya kumaliza kukagua miradi ya maji ambayo wanaitekeleza wilayani Shinyanga.
 
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
 
Soma pia :

About the author

mzalendoeditor