Uncategorized

TANGA UWASA YATUMIA BILIONI 22.2 UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KATIKA KIPINDI CHA AWAMU YA SITA INAYOONGOZWA NA RAIS SAMIA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa taarifa ya
miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha Utawala wa Rais wa awamu ya
Sita Samia Suluhu kwa mkoa wa Tanga

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa taarifa ya
miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha Utawala wa Rais wa awamu ya
Sita Samia Suluhu kwa mkoa wa Tanga ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maji

Meneja
wa Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandis Rashid Shabani akizungumza na
waaandishi wa habari leo wakati wa ziara yao ya kutembelea vyanzo vya
maji eneo la Mabayani na Kituo cha Kutibu Maji cha Mabayani ikiwa  ni
ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maji

 

Afisa
Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akisisitiza jambo wakati wa
mkutano huo kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly

Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akizungumza na waandishi wa habari

Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa eneo la bwala la Mabayani ambalo ndio chanzo cha Maji

Sehemu ya bwawa la Mabayani kama linavyoonekana

NA OSCAR ASSENGA,TANGA

MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) kati ya mwezi
Machi mwaka 2022 hadi sasa imetumia kiasi cha Bilioni 22,221,342,314
katika utekelezaji wa miradi 10 yenye lengo la kuboresha hali ya
upatikanaji wa huduma za majisafi.

Sambamba na hilo pamoja na
uondoshaji wa majitaka katika maeneo yake ya utoaji wa huduma Jijini
Tanga na Miji ya Pangani na Muheza ambapo miradi hiyo inaendelea
kutekelezwa na imefikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Hayo
yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati akitoa
taarifa ya miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha Utawala wa Rais wa
awamu ya Sita Samia Suluhu kwa waandishi wa habari mkoani Tanga.

Aliitaja
miradi hiyo kuwa ni uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa maji Tanga
awamu ya pili ambapo ujenzi wa mradi ulianza mwezi Agosti 2021 na
unatarajiwa kukamilika Mwezi Agosti mwaka huu na unalenga kuboresha
hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Jiji la Tanga na
miji Jirani ya Kasera Mkinga na Muheza.

Alisema mradi huo
utawezesha wakazi wa Tanga wapatao 382,092 kupata maji safi masaa 24 kwa
siku kutoka wastani wa saa 21 kwa siku

Mhandisi Hilly alisema
pia wanatekeleza mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi Tanga
kukabiliana na (Uviko 19) ambapo unatekelezwa kupitia fedha za miradi ya
kuboresha tahadhari ya ugonjwa wa Uviko 19 ambapo unatekelezwa kwa
lengo la kusogeza huduma ya maji kuwafikia wakazi wa maeneo tajwa
wapatao 7200 ujenzi ulianza Desemba 2021 na utakamilika Aprili 2022.

Hata
hivyo alieleza licha ya mradi huo wanatekeleza ujenzi wa miundombinu ya
maji kuboresha upatikanaji wa maji Mitaa ya mpirani,ndaoya, Kibafuta,
Mleni na Chongoleani ambapo mradi huo umeanza kutoa huduma katika vituo
19 vilivyounganishwa na mtandao wa maji.

“Miradi mingine ni
ujenzi wa Bomba la Maji lenye kipenyo cha DN 300 wenye urefu wa mita
8200 kutoka Mowe hadi Pongwe na umekamilika mwezi Desemba 2021 na kwa
sasa unatoa maji kwa wakazi wa Kata za Mlingano,Ngomeni,Lusanga,Mpapayu
na Genge na wakazi wapatao 10,000 wamenufaika nao ”Alisema

Aidha
Mkurugenzi huo aliutaja pia mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Maji Safi
Mji wa Muheza Mjini na ambapo mkandarasi wa ujenzi huo pamoja na
mzabuni wa kuleta mabomba na viungio wameshapatikana na ujenzi wake
utaanza mwezi machi 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu
huku wakazi 15,700 wakitarajiwa kunufaika.

“Mradi mwengine ni
ujenzi wa miundombinu ya maji safi mji wa Pangani ambapo kwa sasa
mkandarasi wa ujenzi pamoja na mzabuni wa kuleta mabomba na viunganishi
wameshapatikana na ujenzi utaanza mwezi Machi mwaka 2022 na unatarajiwa
kukamilika June 2022 na utaboresha upatikanaji wa maji kutoka masaa sita
kwa siku kufikia masaa 12 kwa siku na kunufaisha wakazi wapatao
37,109”Alisema

“Pia kutakuwa na mradi wa ujenzi wa mabwawa ya
ukusanyaji na kusafisha maji taka Muheza ambapo mji wa Muheza haukuwa na
mfumo huo wa lakini mwaka huu fedha 2021/2022 Serikali imeweza
kutekeleza ujenzi wa mfumo wa kukusanya,kutibu na kusafisha majitaka
ikiwa ni pamoja na kununua gari la kukusanya majitaka toka kwa wakazi wa
Muheza na maeneo Jirani”Alisema

Hata hivyo alisema pia
utekeleza wa ujenzi wa mabwawa ya kukusanya na kusafisha maji taka
Pangani ambapo mji huo haukuwa na na mfumo wa maji taka lakini mwaka huu
wa fedha 2021/2022 Serikali imewezesha ujenzi wa mfumo wa
kukusanya,kutibu na kusafisha majitaka ikiwa ni pamoja na kununua gari
la kukusanya majitaka toka kwa wakazi wa Pangani ambao unawanufaisha
wakazi wote wa Pangani na majirani wapatao 20,400 na mzabuni wa ujenzi
ameshakabidhiwa eneo la ujenzi na mradi unatarajiwa kukamilika mwezi
Agosti mwaka huu.

Akizungumzia miradi mengine alisema kuna
miradi inayotekelezwa kwenye mji wa Tanga ambapo ni usanifu wa mradi wa
miundombinu ya majitaka na usimamizi wa ujenzi ambao utakuwa na manufaa
kutokana na miundombinu iliyopo ilijengwa miaka zaidi ya 60 iliyopita na
hivyo imechakaa na mahitaji na gharama halisi za mradi na mhandisi
shauri (WPCOS Co.Ltd )ameshaanza kazi ya usanifu Tanga Januaria 2022 na
anatajiwa kumaliza mwezi June 2022.

Hata hivyo alisema pia
wanaandaa taarifa ya udhibiti wa athari ya Mazingira na Jamii wakati wa
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka ambapo manufaa
yake ni kwamba mhandisi mshauri (Tansheq Co,Ltd) ameshaanza kazi ya
kutafiti na hatimaye kuandaa taarifa ya athari katika jamii na mazingira
na namna ya kudhibiti zile ambazo zitajitokeza wakati wa ujenzi wa
mradi.

About the author

mzalendoeditor