Uncategorized

TPA TANGA WATUMIA MAONYESHO YA TANZFOOD EXPO 2022 JIJINI ARUSHA KUJITANGAZA

Written by mzalendoeditor


,Afisa
Uhusiano wa TPA Tanga Adam Mshindo akizungumza na wadau mbalimbali
waliotembelea banda lao wakati wa maonyesho makubwa ya Kilimo na Chakula
maarufu kama (TANZ
FOOD EXPO 2022yaliyofanyika Jijiji Arusha

Afisa
Uhusiano wa TPA Tanga Adam Mshindo akizungumza na wafanyabiashara
waliotembelea banda lao wakati wa maonyesho makubwa ya Kilimo na
Chakula maarufu kama (TANZ
FOOD EXPO 2022yaliyofanyika Jijiji Arusha

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari ya Tanzania Tawi la Tanga
wameshiriki maonyesho makubwa ya Kilimo na Chakula maarufu kama (TANZ
FOOD EXPO 2022 huku wakiwataka wafanyabiashara kutoka mkoa ya Kanda ya
Kaskazini kutumia Bandari ya Tanga kutokana na maboresho makubwa
yaliyofanywa na Serikali.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo
ambayo wametumia kama njia ya kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana
kwenye Bandari hiyo ,Afisa Uhusiano wa TPA Tanga Adam Mshindo alisema
Serikali imefanya maboresha makubwa ambayo yataongeza ufanisi mkubwa
katika Bandari hiyo.

Alisema pia wamekwenda kushiriki maonyesho
hayo kutokana na kwamba wao ni wadau wake wanashiriki kwenye maonyesho
hayo wanatumia bandari ya Tanga kusafirisha mizigo yao na kujitangaza.

Awali
akizungumza wakati wa maonyesho hayo Mhandisi kutoka Bandari ya Tanga
Hamisi Kipalu alisema kwa sasa wanaendelea na mradi mkubwa wa uboreshaji
wa Bandari ya Tanga kwa awamu ya pili mradi wa ujenzi wa gati namba
moja na namba mbili wenye urefu wa mita 450.

Alisema ujenzi huo
unatekelezwa na mkandarasi kutoka nchini China akisimamiwa na mwandisi
Mshauri Kampuni ya NIRAS kutoka nchini Denmark akishirikiana na Kampuni
ya Kitanzania NovakKauli hiyo iliungwa mkono pia na Balozi wa Ujerumani
nchini Tanzania Ms Regine Hess ambaye naye aliupongeza mchango wa
bandari katika kuendeleza shughuli mbalimbali ikiwemo za kilimo

Alisema
faida za mradi huo ni kubwa kutokana na kwamba itasaidia kuongeza
ufanisi wa bandari hiyo sambamba na kufungua biashara na kuongeza wateja
kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Maonyesho hayo yalifunguliwa
na Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ambae aliupongeza mchango wa
Bandari katika kuendeleza kilimo na kufikisha mazao katika masoko ya
kitaifa na kimataifa.

RC Mongela alisema maonyesho hayo ambayo
yalifanyika kwa siku tatu kwenye viwanja vya Magereza Kisongo mkoani
humo yalitoa fursa atengea muda waje kupata elimu ya bure na inafaida
kubwa sana

Hata hivyo Mratibu wa Maonyesho hayo Dominiki Shoo
alisema maonyesho hayo yatakuwa yanafayika kila mwaka na lengo kufungua
milango kwa wakulima.

About the author

mzalendoeditor