Featured Michezo

PARTEY,LACAZETTE WAIMALIZA LEICESTER CITY

Written by mzalendoeditor

Timu ya Arsenal imeendeleza kasi ya kusaka nafasi ya  kuingia nne bora baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester City mchezo wa Ligi ya Uingereza katika Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na kiungo Mkabaji Thomas Partey dakika ya 12 pamoja Alexandre Lacazette alifunga bao la pili kwa Penalti dakika ya 59.

Kwa ushindi huo Arsenal imefikisha pointi 51 na kurejea nafasi ya nne, wakati Leicester inabaki na pointi zake 33 za katika nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 26.

About the author

mzalendoeditor