Muonekano wa vitoto vichanga vikiwa vimefariki baada ya kutupwa kwenye ghuba la uchafu na mama yao ambaye bado hajafahamika eneo la Majengo Makaburini Manispaa ya Shinyanga.
Baadhi ya Wananchi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio wakishuhudia vitoto hivyo vichanga vikiwa vimefariki baada ya kutupwa na mama yao kwenye Ghuba la uchafu lililopo Majengo Makaburini Manispaa ya Shinyanga.
……………………………………………..
Na Marco Maduhu, SHINYANGA 
  
WATOTO wachanga ambao ni mapacha, wamefariki dunia baada ya mama yao ambaye bado hajafahamika, kuvitupa katika eneo la kuhifadhia uchafu (ghuba) lililopo Mtaa wa Majengo Makaburini Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.

Tukio hilo limetokea usiku wa kumkia leo, ambalo limeguduliwa majira ya saa 12 alfajiri na waokota uchafu kufika kwenye Ghuba hilo, na kuanza kutafuta mali mbalimbali ndipo walipofunua mfuko mmoja wakijua huenda kunavitu vizuri na kukuta vichanga hivyo ambavyo ni mapacha vikiwa tayari vimefariki.

Mmoja wa majirani wa eneo hilo la kuhifadhia uchafu Costantine Samweli, alisema mara baada ya waokota uchafu kuona vichanga hivyo vimekufa, ndipo wakaanza kupiga kelele na wao wakatoka kushuhudia tukio hilo na kuvikuta ndani ya mfuko vikiwa vimeshafariki.

“Ukiviangalia vizuri vichanga hivi huyu mama alivitoa vikiwa bado havijafikisha miezi Tisa, sababu hapa pembeni kama unavyoona kuna Sindano na baadhi ya vitu ambavyo vimetumika kumtolea watoto hawa,”alisema Samweli.

Nao baadhi ya akina mama ambao walifika eneo hilo la tukio, kwa nyakati tofauti walilaana kitendo hicho huku wengine wakiangua kilio, na kuiomba Serikali imtafute mwanamke ambaye amefanya unyama huo, na wamchukulie hatua kali za kisheria na liwefundisho kwa wengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Majengo Majid Issa, alisema tukio kama hilo la kutupa vitoto vichanga katika ghuba hilo la uchafu ni la pili, na kutoa wito kwa wanawake kama mimba zao au watoto wanakataliwa na wanaume wasiwafanyie ukatili, bali wawapeleke kwenye vituo vya malezi ya watoto.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha wanafanya uchunguzi ili kumbaini mwanamke aliyefanya unyama huo.
 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Previous articlePARTEY,LACAZETTE WAIMALIZA LEICESTER CITY
Next articleTASAC YATAKA WAFANYABIASHARA MPAKANI KUACHA KUTUMIA NJIA ZA PEMBENI KUPITISHA MIFUGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here