Featured

KAMATI YA PAC YATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA MAJI IKUNGI -SINGIDA

Written by mzalendoeditor

Mjumbe wa Kamati Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Isack Kamwelwe akohoji jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa Kituo kidogo cha kusambaza umeme Singida, Kamati hiyo ipo Mkoani Singida kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC) wakimsikiliza Meneja wa kusimamia ujenzi katika vituo vya umeme kutoka Shirika la Umeme (TANESCO) Ndugu Timothy Mgaya, wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa Kituo kidogo cha kusambaza umeme Singida, Kamati hiyo ipo Mkoani Singida kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali(PAC), wakimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kituo kidogo cha kusambaza umeme Singida kutoka Shirika la Umeme (TANESCO) Ndugu Emmanuel Manilabona, wakati Kamati  ilipotembelea na kukagua mradi wa Kituo hicho, Kamati hiyo ipo Mkoani Singida kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singinda, Mhe. Jerry Muro akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ilipowasili katika eneo la mradi wa maji Ikungi unaotekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka ipo Mkoani Singinda kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC) wakimsikiliza Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida, Lucas Said akielezea utekelezaji wa mradi wa maji Ikungi wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo. Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka ipo Mkoani Singinda kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Kamati Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akieleza jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea eneo la mradi wa maji Ikungi unaotekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Kamati hiyo ipo Mkoani Singinda kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali.

 PICHA NA OFISI YA BUNGE

About the author

mzalendoeditor