Na.WAF-Dar ea Salaam
Viongozi na watumishi wa Wizara ya Afya wametakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kuzingatia taaluma zao ili kuweza kuleta tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akiwasilisha mada ya Utawala Bora na Uongozi katika utumishi wa umma kwenye Mafunzo Elekezi kwa Viongozi na wajumbe wa menejimenti ya Wizara ya Afya.
Dkt.Ndumbaro amesema kuwa kama watumishi wa umma wanapaswa kuelewa maadili ya utumishi wa umma pamoja na mfumo mzima wa utumishi wa umma
Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema katika utumishi wa umma kuna wajibu kadhaa wa viongozi hivyo kila wanachofanya wanapaswa kutanguliza maslahi ya nchi,kuipenda nchi na kuwa wazalendo pamoja na kuwa na moyo wa kujitolea katika kufanya majukumu kwa lengo la kuipenda nchi yao.
“Mnapaswa kufanya kazi kwa juhudi na kutekeleza kazi mlizopangiwa ili kuweza kutimiza malengo na malengo yapatikane”.Alisisitiza Dkt. Ndumbaro
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watendaji hao kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuwasikiliza na kutumia lugha yenye staha.
Vilevile aliwataka watendaji hao kufanya kazi kwa kasi na matokeo yaonekane pamoja na kuakisi utumishi wa umma.
Mafunzo hayo yaliyowajumuisha Wakurugenzi,Wakurugenzi Wasaidizi,Wakuu wa Vitengo,Wasajili wa Mabaraza na Bodi za kitaaluma,Mameneja wa Miradi pamoja na baadhi wa watumishi wa wizara hiyo