Featured Kitaifa

SIRRO ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WAHALIFU WA UPORAJI NA UVUNJAJI

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameagiza kufanyika kwa Operesheni za kuwasaka na kuwakamata wahalifu wanaotumia pikipiki kupora pamoja na wahalifu wanaojihusisha na uvunjaji na kuiba mali za wananchi.

IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ukaguzi wa ghafla kwenye kituo cha Polisi Stakishari, Tabata Shule na Kawe Jijini Dar es salaam, ambapo kwenye ukaguzi huo amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji Kata na Polisi Kata kuendelea kuhamasisha Vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha matukio ya uhalifu yanapungua kwenye maeneo yao.

Aidha, IGP Sirro amewataka madereva hasa wa pikipiki maarufu bodaboda kufuata masharti ya leseni zao na kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu wa kutumia nguvu.

About the author

mzalendoeditor