Uncategorized

RC MTAKA AAGIZA VIONGOZI KUANDAA SHERIA NDOGONDOGO KULINDA MIUNDOMBINU YA ANWANI ZA MAKAZI

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa uwekaji wa alama za mitaa, barabara pamoja na vibao vya namba za nyumba wilayani Bahi Mkoani Dodoma.

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda,akizungumza wakati wa uwekaji wa alama za mitaa, barabara pamoja na vibao vya namba za nyumba zoezi lililofanyika wilayani humo.

Mbunge wa jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo,akizungumza wakati wa uwekaji wa alama za mitaa, barabara pamoja na vibao vya namba za nyumba zoezi lililofanyika wilayani humo.

……………………………………….

Na.Bolgas Odilo,BAHI

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amewaagiza viongozi wa Halmashauri zote za mkoa wa Dodoma kuandaa sheria ndogondogo ambazo zitatumika kulinda miundombinu ya anwani za makazi ambazo zinawekwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kauli hiyo aliitoa  wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati akizindua uwekaji wa alama za mitaa, barabara pamoja na vibao vya namba za nyumba.

Mtaka amesema kuwa  pamoja na wilaya zote za mkoa wa Dodoma kuanza kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan katika uwekaji wa anwani za makazi lakini ipo haja ya kutungwa kwa sheria ambazo zitasaidia kulinda miundombinu hiyo.

“Lazima wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na baraza la madiwani kuona ni jinsi gani mnaanza kuandaa sheria ndogondogo zitakazo linda miundombinu hii ili yeyote atakaye bainika kung’oa vyuma hivi vyenye majina na mitaa na kwenda kuviuza kama vyuma chakavu kukamatwa na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.

“Hivi vyuma ambavyo tunatumia kuweka majina ya mitaa ni nyara za wilaya hivyo kwa yeyote atakaye bainaka kuiba ni lazima tuwe na sheria ya kuwabana aliyeuza na aliyenunua”alisema Mtaka

Hata hivyo Mtaka amesema kuwa  hali hiyo ya kutungwa kwa sheria itasaidia kuondokana na adha ambazo wakala wa barabara nchini Tanroad wanakumbana nao wa watu kuiba alama za barabarani.

“Unakuta kuna alama zimewekwa na Tanroad kuwa hapa kuna kivuko cha mifugo watu wanag’oa na kwenda kuuza vyuma chakavu sasa hivi ambavyo tunaviweka hapa leo lazima tuvitungine sheria kuvilinda”amesema

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda,amesema kuwa mpango huo wa uwekaji anwani za makazi wanatarajia kukamilisha ndani ya wiki mbili kuanzia sasa katika vijiji vyote 59.

About the author

mzalendoeditor