Featured Kitaifa

WAZIRI GWAJIMA AITAKA MEWATA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WIZARA YAKE

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama Cha Madaktari Wanawake (MEWATA) uliofanyika leo Februari 25,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akieleza jambo kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama Cha Madaktari Wanawake (MEWATA) uliofanyika leo Februari 25,2022 jijini Dodoma.

BAADHI ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama Cha Madaktari Wanawake (MEWATA) uliofanyika leo Februari 25,2022 jijini Dodoma.

Rais wa Chama Cha Madaktari Wanawake (MEWATA) Dkt. Mary Charles,akielezea lengo la Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama hicho  uliofanyika leo Februari 25,2022 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya TAMISEMI, Dkt. Grace Magembe,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Waziri  wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) mara baada ya kufungua  Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama Cha Madaktari Wanawake (MEWATA) uliofanyika leo Februari 25,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama Cha Madaktari Wanawake (MEWATA) uliofanyika leo Februari 25,2022 jijini Dodoma.

………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,DODOMA

Chama Cha Madaktari Wanawake (MEWATA) wametakiwa kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalumu katika kuelimisha jamii ifanye maamuzi sahihi kuhusu masuala mbalimbali ya afya hususan kuhamasisha na kuelimisha jamii kupata Chanjo ya UVIKO-19.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 25,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 19 wa MEWATA, unaongozwa na kaulimbiu “Kuimarisha uchanjaji wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 miongoni mwa Madaktari Wanawake Tanzania”.

Waziri Gwajima amesema mkutano huo umefanyika muda muafaka, kwa kuwa mpaka sasa bado Dunia inaendelea kutekeleza jitihada mbalimbali za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Korona ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu ulimwenguni.

“MEWATA juhudi za kukabiliana na UVIKO-19 zinahusisha Wadau mbalimbali wakiwemo wanawake kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi yao katika jamii hivyo, kwa mantiki hii, ushirikiano wa wataalamu wa sekta mbalimbali ikiwemo Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii hususan wataalamu wanawake ni muhimu kwani wao kuwa mstari wa mbele itaongeza tija zaidi”. Ameeleza Dkt. Gwajima.

Hata hivyo Dkt. Gwajima ameeleza kuwa MEWATA yenye wataalamu wanawake ikishirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii itaweza kufikisha ujumbe wake kwenye jamii kwa ufanisi zaidi na siyo tu kwa UVIKO -19 bali hata kwa mambo mengine yanayohusu changamoto za afya ili jamii ielewe kwa lugha nyepesi zaidi ya wataalamu wa maendeleo na ustawi wa jamii walioshirikiana na MEWATA

“Ninatambua kuwa bado kuna wananchi wengi ambao bado hawajapata elimu ya kutosha ya CHANJO ya UVIKO-19 pamoja na elimu juu ya masuala mengine ya afya hivyo, tuendelee kushirikiana na kuwafikia kwa kuwapa elimu ya kutosha kuhusu chanjo na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa ujumla pamoja na elimu ya afya juu ya magonjwa mbalimbali na mila potofu za jamii zinazopelekea kuathiri afya hasa kwa watoto na wanawake”, amesisitiza DKt. Gwajima

Dkt. Gwajima amesema kwa MEWATA ambao tayari wamepata elimu ya kutosha na kuchanja na kwa nafasi zao kama wataalamu wanawake, amewataka kuwa mabalozi wazuri wa kuhakikisha kuwa wanaendeleza jitihada za kuwafikishia elimu hii wale ambao bado hawajafikiwa hususan wanawake ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kujikinga kwa kupata chanjo ya UVIKO 19 wao na familia zao.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya TAMISEMI, Dkt. Grace Magembe amesema kuwa wanamshukuru Rais Mhe. Samia  kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya na kuipa kipaumbele katika maswala ya lishe,afya tiba, afya kinga na eneo la mama na mtoto.

“Sisi kama Madaktari Wanawake Tanzania tunajukumu kubwa la kutoa elimu kwa jamii kwa maana ya kubadilisha fikra potofu na kuwafikishia huduma bora wananchi”, amesisitiza Dkt. Magembe

Naye Rais wa MEWATA Dkt. Mary Charles ameeleza lengo kuu la mkutano huo kuwa ni kuhamasisha Madaktari Wanawake kuwa mabalozi kwa wananchi juu ya kupata chanjo ya Uviko 19.
Dkt. Mary amesema kuwa pia mkutano huo unalenga kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao.

About the author

mzalendoeditor