Featured Kitaifa

WAZIRI BASHUNGWA AZIELEKEZA HALMASHAURI KUTENGA MAENEO YA UWEKEZAJI

Written by mzalendoeditor

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa Akijimaswali hayo amesema ni lazima Halmashauri kutenga maeneo maalumu  kwa ajili ya uwekezaji na vikundi vinavyokopa asilimia 10 ya fedha za halmashauri kuwa Moja wa wanufaika wa maeneo hayo.

Haya yameelezwa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali, Mhe. Innocent Bashungwa wakati akitoa ufafanuzi kutokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo, Charles Kimei

Mbunge Kimei alitaka kujua kama Ofisi ya Rais-TAMISEMI haioni umuhimu wa kuziwezesha halmashauri kutenga maeneo mahususi kwa wajili ya wajasiliamali na kuyawekea miundombinu stahiki ili wanufaika wa fedha za asilimia 10 za halmashauri wakatumia maeneo hayo kufanya shughuli zao.

Pia alitaka kujua kama Wizara haioni haja ya kushirikiana na SIDO kwenye utoaji wa mikopo ya halmashauri hasa ikizingatia kuwa fedha zinazokopewa na SIDO zimekuwa zikirejeshwa Kwa zaidi ya asilimia 90.

Akijibu maswali hayo, Bashungwa alisema ni la Zima Halmashauri kutenga maeneo maalumu  kwa ajili ya uwekezaji na vikundi vinavyokopa asilimia 10 ya fedha za halmashauri kuwa Moja wa wanufaika wa maeneo hayo.

” Mhe Mbunge(Charles Kimei)  tukuhakikishie hili tumeboresha zaidi, tumeshaka na Wizara ya Kilimo kuangalia makundi ya vijana wasomi ambao wanapata asilimia 10 ya fedha za halmashauri zetu, majiji na manispaa namna bora ya kuweza kuwasaida maeneo mahususi kama haya. Hoja kama hii tunaifanyia kazi.”

Bashungwa alitumia fursa hiyo kuzielekeza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatekekezwa maagizo ya Serikali ya kutenga maeneo mahususi kwa ajili ya uwekezaji.

Aidha, Bashungwa alisema kwa sasa Ofisi ya Rais-TAMISEMI inashirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuratibu suala la utengaji wa maeneo ya uwekezaji.

” Tunashirikiana na wenzetu wa ardhi kuratibu hili vyema kwasababu yako mambo ya fidia halmashauri zingine zinanzia ya kutenga maeneo lakini wanakosa fedha Kwa ajili ya fidia kwa hiyo yote haya tunaangalia ndani ya serikali kuhakikisna maeneo haya pia.

Kuhusu kutoaji mikopo na upotevunwa fedha, Bashungwa alisema  Ofisi ya Rais-TAMISEMI  kwa kushirikiana na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara zinaangalia namna ya kuhakikisha fedha asilimia 10 kutoka kwenye halmashauri na za mifuko mingine ndani ya  serikali kunakuwa na namna bora ya kuzipeleka kwenye makundi ili iweze kuleta tija

About the author

mzalendoeditor