Featured Kitaifa

DKT.NCHIMBI AMSHUKURU DKT.MPANGO KWA MCHANGO WAKE KATIKA AWAMU YA SITA

Written by Alex Sonna

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiombewa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.

….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempongeza na kumshukuru Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa mchango aliyoutoa wakati wa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Makamu wa Rais, yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Amesema kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita, ambayo ilitoa urahisi wakati wa ufanyaji kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Makamu wa Rais amesema ataendeleza jukumu la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwezo wake wote ili kutekeleza vema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuwaletea wananchi maendeleo.

Pia amemsihi, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Philip Mpango kuendelea kutoa mchango wake pale utakapohitajika, katika utekelezaji wa sera mbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwemo masuala ya uchumi wa buluu.Β 

Kwa upande wake Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa nafasi hiyo muhimu na kumsihi kutekeleza vema majukumu ya kuwa mshauri namba moja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemsihi kutumia hekima na unyenyekevu wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, wakati alipowasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, kwaajili ya makabidhiano ya Ofisi, leo tarehe 04 Novemba 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa nyaraka mbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Rais, kutoka kwa mtangulizi wake, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiombewa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akigana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja mara baada ya makabidhiano ya Ofisi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 04 Novemba 2025.

Β 

About the author

Alex Sonna