Kaimu Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Aksa Mhando,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446,kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma.
NaAlex Sonna – DODOMA
WIZARA ya Katiba na Sheria imezitaka taasisi za habari nchini kutumia kalamu zao kusaidia kuelimisha jamii kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446, ambayo inalenga kulinda usalama wa watu wanaojitokeza kwa ujasiri kutoa taarifa au ushahidi dhidi ya uhalifu, rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Akifungua kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria hiyo leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Aksa Mhando,amesema kuwa Sheria hiyo ni nyenzo muhimu katika kujenga imani ya wananchi kwa mifumo ya haki na kuimarisha utawala wa sheria nchini.
“Sheria hii inalenga kuhakikisha kuwa wale wanaojitokeza kutoa taarifa au ushahidi dhidi ya makosa mbalimbali wanapata ulinzi wa kisheria, kiusalama na kijamii. Ni sheria inayojenga imani ya wananchi katika mifumo ya haki na kuimarisha misingi ya uwajibikaji,” amesema Bi.Mhando
Amesema kuwa vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuelimisha umma kuhusu sheria hiyo ili kuondoa hofu kwa wananchi wanaotaka kufichua uhalifu, kwani taarifa wanazotoa zitahifadhiwa kwa usiri mkubwa na zitatumika bila kuwataja watoa taarifa.
“Vyombo vya habari ni daraja kati ya Serikali na wananchi ni sauti inayowezesha taarifa sahihi kufika kwa umma na kuchochea mabadiliko chanya katika jamii,” amesisitiza.
Bi.Mhando amebainisha kuwa kupitia kikao hicho, washiriki watapata uelewa wa kina wa Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi na Kanuni zake zilizotangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 59 la Februari 10, 2023, sambamba na kutengeneza mkakati wa kitaifa wa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa sheria hiyo.
Aidha,amefafanua kuwa kanuni hizo zimeweka utaratibu wa kutoa motisha kwa wale ambao taarifa zao zitasaidia kuokoa mali ya umma, kupatikana kwa wahalifu au kulinda maisha ya watu kutokana na uhalifu uliopangwa.
“Wale ambao taarifa zao zitafanikisha kuokoa mali ya umma au kulinda maisha ya watu wamewekewa utaratibu wa kupatiwa motisha, ikiwa ni pamoja na fidia kwa wale watakaopata madhara kutokana na taarifa walizotoa,” ameongeza Bi.Mhando
Hata hivyo amesema kuwa Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika utoaji wa elimu ya kisheria ili kujenga uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao, sambamba na kuimarisha ushiriki wa jamii katika mapambano dhidi ya uhalifu.
“Ushirikiano wenu ni muhimu katika kuhakikisha kuwa uelewa wa sheria hii unafika katika kila kona ya nchi kupitia redio, televisheni, magazeti, na majukwaa ya kidijitali,” amesema
Kikao hicho cha siku mbili kinatarajiwa kuibua mikakati na maoni ya wadau wa habari kuhusu njia bora za kuelimisha umma na kuimarisha usalama wa watoa taarifa na mashahidi nchini, ili kujenga jamii yenye ujasiri, uwazi na uwajibikaji.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Aksa Mhando,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446,kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma. 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Aksa Mhando,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446,kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Aksa Mhando (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446,kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Aksa Mhando,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446,kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Judica Emanuel Nkya,akiwasilisha mada kuhusu sheria ya watoa taarifa na Mashahidi,Sura ya 446 wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma.

Wakili wa Serikali Daraja la I Bw.Amani Manyaga,akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za watoa taarifa na Mashahidi Tangazo la Serikali Namba 59 la tarehe 10 Februari,2023 wakati wa kikao kazi cha siku mbili cha vyombo vya habari kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi kilichoanza leo Oktoba 27,2025 jijini Dodoma.