Featured Kitaifa

POLISI SONGWE YAPEWA MAGARI MAWILI YA KISASA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA

Written by Alex Sonna
Na Issa Mwadangala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga, amekabidhi magari mawili mapya aina ya Robur Armored TLC300 kwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Songwe kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura.Makabidhianao hayo yamefanyika Oktoba 23, 2025, katika ofisi ya Kamanda Mkoa wa Songwe iliyopo Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoani humo na mara baada ya kukabidhi magari hayo, SACP Senga alitoa shukrani za dhati kwa IGP Camillus Wambura na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha uwezo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kupitia upatikanaji wa vitendea kazi vya kisasa, huku akisema kuwa magari hayo yataongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku hususan katika kudhibiti ghasia, kulinda raia na mali zao, pamoja na kuimarisha amani na utulivu Mkoani humo.

Aidha, Kamanda Senga amesisitiza dhamira ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kuhakikisha magari hayo yanatumika ipasavyo na yatatunzwa kwa uangalifu mkubwa ili yaweze kutumika kwa muda mrefu na Mkoa wa Songwe kuendelea kuwa salama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Songwe, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Sija Kadogosa, ameahidi kutekeleza kwa vitendo maelekezo yote yaliyotolewa kuhusu matumizi ya magari hayo ili yawe chachu ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe.
IMG-20251023-WA0084-2.jpg
SACP Senga akimkabidhi funguo za Gari hizo  SSP Kadogosa 
IMG-20251023-WA0083-2.jpg
KAMANDA Senga akiwa na  SSP Kadogosa na Madereva wa Magari hayo.

About the author

Alex Sonna