Featured Kitaifa

DK. NTULI ASISITIZA USIMAMIZI WA FEDHA ZA DAWA MIKOANI

Written by mzalendoeditor

OR-TAMISEMI

Mkurugenzi wa Idara ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Ntuli Kapologwe ameitaka  Timu ya usimamizi wa  shughuli za Afya (CHMT) katika Mikoa yote Tanzania bara kuimarisha usimamizi wa fedha za dawa walizopokea kwa mwaka wa fedha 2021/22.

 Amesema fedha hizo zisimamiwe ipasavyo ili hizo zitumike  katika kuboresha upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma  ya afya  lakini pia zitumike kukuza mtaji utaotumika katika  ununuzi wa  dawa na vifaa tiba.

Dkt. Ntuli ametoa kauli hiyo Mkoani Kigoma April 25,2022 wakati wa ukaguzi shirikishi Mkoani humo na ambapo Mkoa huyo ulipokea Shilingi Bil 2.7 kutoka Serikali  kuu kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajiki ya ununuzi wa dawa.

“Fedha hizo ni Revolving Fund inatakiwa kuzunguka na Shilingi Bil. 2.7 ni fedha nyingi mno kwa Mkoa mmoja, CHMT niwaombe hakikisheni mnasimamia kikamilifu fedha hizi ili tuondokane na madeni ya dawa lakini pia zikizungushwa vizuri tutapata faida ya mtaji ambao utaendelea kuboresha utoaji wa  huduma  ya afya”Amesema Ntuli.

Aidha  amewataka Makatibu afya na Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia stahiki za watumishi wa Idara ya afya  ikiwemo stahiki ya kupandishwa madaraja ili kuleta motisha na kuongeza tija katika utendaji kazi. 

“ Lazima tuwatengenezee  mazingira  mazuri  watu ambao  tunafanya nao  kazi ili kuwaongezea ari katika utekelezaji wa majukumu  yao ya kutoa  huduma  kwa  wananchi” Amesema Ntuli

Pia  ameishauri CHMT  kutembelea  na kuimarisha usimamizi katika utekelezaji  wa mindombinu ya kutolea huduma  za afya huku ikizingatia ushirikiano katika uandaaji wa taarifa  za  utekelezaji wa miundombinu hiyo.
Aidha Ntuli  amempongeza Mganga  Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Waganga Wakuu wa Wilaya katika   kuwatambua watu wenye ulemavu wapatao 16,088 katika Mkoa wa Kigoma na kuunda kamati 491 za watu wenye uemavu. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Lebba ameahidi kushirikiana na CHMT katika kushughulia mapungufu yaiyobainishwa katika kikao hicho ili kuboresha utoaji wa huduma ya afya katika Mkoa wa Kigoma.

About the author

mzalendoeditor