Featured Kitaifa

BABA WA KAMBO ADAIWA KUMCHEZEA SEHEMU ZA SIRI MTOTO WA MIEZI 11 TANGA

Written by mzalendoeditor

JESHI la Polisi mkoani Tanga limethibitisha kutokea tukio la mtoto wa miezi 11 kupitishiwa kuchezewa sehemu za siri na baba yake wa kambo anayeishi eneo la Amboni Jijini Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo alisema tukio hilo lilitokea Aprili 17 mwaka huu  katika eneo la Amboni ambapo mtoto huyo alichezewa sehemu za siri na baba yake wa kambo.

Akizungumzia namna tukio hilo lilivyotokea Kamanda Jongo alisema mtoto huyo alikuwa amebebwa mgongoni na mama yake huku baba yake kwa sababu michezo hiyo alikuwa ameizoea akampitia mtoto kwa kumpitishia kidole sehemu za siri .

Kamanda Jongo alisema baada ya tukio hilo mama huyo alitoa taarifa kituo baada ya uchunguzi wa daktari ikathibitika ni kweli mtoto sehemu za siri zipo wazi ingawa hajaingiliwa kimwili maana yake yule mtoto amezoeleka kuchezewa.

“Kwa hiyo baba huyo hatua za kisheria zinaendelea kwa lengo la kuhakikisha mtuhumiwa anachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuwa fundisho kwa watu wenye tabia za namna hiyo”Alisema.

Hata hivyo alisema matukio kama hayo na mengine yamekuwa yakiendelea kujitokeza mara kwa mara watoto wa kike ukatili wa kijinsia watoto wadogo wanaingiliwa watoto wa kike kupata ujauzito chini ya umri wao.

“Kwani kuna tukio Handeni mtoto wa darasa la sita amepata ujauzito na matukio yanayofanana na hayo niwaambie wananchi sitavumilia matukio ya namna hiyo kwenye mkoa  nitahakikisha kila wanaohusika na matukio hayo wanachukuliwa hatua kali za kisheria”Alisema RPC Jongo.

About the author

mzalendoeditor