Baadhi ya watumishi wanawake wa Wizara ya Fedha, wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, yaliyoadhimishwa kitaifa Jijini Arusha, yenye kaulimbiu ya ‘’Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji’’.
……
Wizara ya Fedha imeungana na Watanzania wengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, iliyofanyika kitaifa Jijini Arusha, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza maadhimisho hayo yakiwa yamebeba kauli mbiu ya ‘’Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji’’.
Baadhi ya watumishi wanawake wa Wizara ya Fedha, wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, yaliyoadhimishwa kitaifa Jijini Arusha, yenye kaulimbiu ya ‘’Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji’’.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (kushoto), akitoa elimu ya fedha kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara, katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amiri Abeid, jijini Arusha.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Usimamizi Rasilimali Watu Wizara ya Fedha, Bi. Fauzia Nombo (wa tatu kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (wa nne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha katika Banda la Wizara ya Fedha, wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amiri Abeid, jijini Arusha.
Maafisa Hesabu Wakuu, Kitengo cha Huduma za Mfuko Mkuu (CFS), Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky na Bi. Mercelina Haule, wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amiri Abeid, jijini Arusha
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)