Featured Kitaifa

BINTI WA MIAKA 17 AJIUA KWA CHANDARUA BAADA YA KUACHIKA MARA TATU

Written by mzalendoeditor
Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Rebecca Benjamin, Mkazi wa Kata ya Izunya, Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, mwenye umri wa miaka 17, amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kile kinachoelezwa kuwa ni msongo wa mawazo baada ya kuolewa na kuachika mara tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema mwanamke huyo alikutwa amejinyonga kwa kujining’iniza kwenye kenchi la nyumba aliyokuwa anaishi kwa kutumia kamba iliyosokotwa kwa chandarua kutokana na msongo wa mawazo.
Kamanda Mwaibambe ameyasema hayo alipokutana na kamati ya amani na maadili ya Mkoa wa Geita uliokuwa na lengo la kutokomeza matukio ya watu kuua na kujiua.

About the author

mzalendoeditor