Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA AZINDUA UGAWAJI WA VIFAA VYA TEHAMA VYA ELIMU MSINGI, WATHIBITI UBORA NA VYUO VYA UALIMU.

Written by mzalendoeditor

    

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WIZARA ya Elimu imezindua Vifaa jumla ya kompyuta 3,354 ambapo kati ya hizo Laptop ni 1637 na Deskotop  kompyuta ni  1717, printer 12, projector 12 na internet switches 12 vikiwa vimenunuliwa na Serikali pamoja na wadau wa Elimu ili kuunga jitihada za awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hasan ya kuwekeza kwenye Elimu.

Akizungumza katika hafla hiyo  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema komputa zinazozinduliwa, laptop 1337 zinatokana na program Covid Recovery ambao ni mradi wa kuboresha mazingira Salama ya Kujilinda na Maambukizi ya Virus vya CORONA.

“Komputa hizi zitagawiwa kwa Maafisa Uthibiti ubora na Maafisa Elimu Kata ili kuboresha utendaji kazi wao Komputa Mpakato na TEHAMA zitasaidia Kurahisisha Utendaji wa Kazi, Utunzaji na uchakataji wa Taarifa na Takwimu na zitapunguza gharama ya viandikia kwakuwa taarifa zinaweza kupatikana katika nakala laini”. Amesema Prof.Mkenda

Aidhaa ametoa pongezi kwa Shirika la “Digital Pipeline” la nchini Uingereza kwa kukubali kushirikiana na Serikali katika kuendeleza Matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na Ujifunzaji kwenye shule zetu. 

Hata hivyo Prof. Mkenda ametoa wito kwa wadau wengine wa Elimu, kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta mabadiliko chanya hasa katika matumizi ya teknolojia katika elimu yetu.

“Serikali yetu kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, itaendelea kutoa ushirikiano uliotukuka kwa kila mdau katika eneo ambalo anaweza kushirikiana na Serikali kuendeleza Elimu yetu”. Amesema

About the author

mzalendoeditor