Featured Kitaifa

NAIBU KATIBU MKUU JENIFA OMOLO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA 2024

Written by mzalendo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akisikiliza maelekezo  kutoka kwa Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Maendaenda, kuhusu namna mfumo wa GePG unavyofanyakazi, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam
 
Wananchi wametakiwa kulipa kodi kwa hiari kwa kutambua kuwa Serikali haiwezi kutekeleza miradi ya maendeleo bila kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo mbalimbali zikiwemo shughuli za kila siku za mtu mmoja mmoja.
 
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipotembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam. 
 
Bi. Omolo alisema kuwa, miundombinu wezeshi ambayo inachochea maendeleo na kukuza pato la nchi na mtu mmoja mmoja inatokana na fedha zinazokusanywa kupitia kodi na shughuli nyingine.
 
Kwa upande mwingine ametaja huduma zinazopatikana katika Banda la Wizara ya Fedha kuwa ni pamoja na elimu kuhusu Bajeti ya Serikali, Sera, uwekezaji, pensheni na mirathi, ununuzi wa umma na ugavi, vyuo vya elimu ya juu, mifumo ya fedha, takwimu, rufaa za kodi, usuluhishi na huduma za kibenki.
 
Aidha amevipongeza vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Fedha kwa kuendeleza bunifu mbalimbali kupitia vijana, ambapo ameutaka uongozi wa vyuo hivyo kuwaendeleza na pia kufanya tafiti ili kutataua changamoto za wananchi. 
 
Bi. Omolo amewataka wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Fedha ili kuweza kupata uelewa wa huduma na majukumu ya Wizara ya Fedha na taasisi zake ili ziweze kuwasaidia katika majukumu yao.
 
Amesema watoa huduma katika Banda la Wizara ya Fedha wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa huduma stahiki kwa wananchi watakao tembelea Maonesho ya ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).  
 
Naibu Katibu Mkuu Jenifa Omolo ametembelea Idara, Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Emmanuel Tutuba, baada ya kutembelea Banda la BOT, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akisikiliza maelekezo  kutoka kwa Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha, Bw. Emmanuel Maendaenda, kuhusu namna mfumo wa GePG unavyofanyakazi, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akisoma kipeperushi kinachoelezea huduma za Kitengo cha Maktaba cha Wizara ya Fedha, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akimsikiliza kwa Umakini Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Kitengo cha Pensheni, Bi. Joyce Chacky, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akimsikiliza kwa Umakini Afisa Mahusiano wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Bi. Sarah Goroi, wakati alipotembelea Chuo hicho katika Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akimsikiliza kwa Umakini,  Mtaalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. Stanley Jackson ,wakati alipotembelea Taasisi hiyo katika Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akisikiliza maelekezo  kutoka kwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) alipotembelea banda la Benki hiyo, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
 
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

About the author

mzalendo