Featured Kitaifa

TCB YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KWA KULETA HUDUMA ZA KIBUNIFU KIDIGITAL .

Written by mzalendoeditor

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) inajivunia kuwa moja ya washiriki wa maonyesho yanayoendelea ya SABASABA, ambayo yamezinduliwa na Mheshimiwa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kwani Maonyesho ya SABASABA ni tukio kubwa la kipekee nchini linalotoa fursa ya kutangaza bidhaa na huduma za sekta mbalimbali.

Maonyesho hayo yenye Kauli mbiu isemayo Tanzania ni mahali salama pa biashra na uwekezaji ni jukwaa la kipekee kwa biashara kujitangaza, kutafuta fursa za masoko na kuzindua bidhaa mpya sokoni Uwepo wa Mheshimiwa Rais katika maonyesho ya mwaka huu unadhihirisha dhamira thabiti ya Serikali yake katika kukuza na kuimarisha uchumi, na kuboresha mazingira ya ustawi wa biashara ili kuchangia katika maendeleo ya nchi.

Kwa kutambua hilo Benki ya TCB ambayo ni taasisi ya kifedha inayoongoza kwa kutoa bidhaa bunifu za kifedha zinazokidhi mahitaji ya wateja wake imlenga kuongeza ujumuishi wa kifedha na kuimarisha uchumi, huku ikikusudia kuchangia katika ujenzi wa uchumi na kuongeza pato la taifa .

Aidha TCB imetambua fursa inayoletwa na maadhimisho hayo na hivyo , benki imeimarisha nafasi yake katika ushindani wa soko kwa kutangaza bidhaa zake mpya za kidigitali ambazo zimebuniwa ili kukidhi mahitaji ya wateja yanayoendelea kubadilika kila maisha ya watanzania ambazoi ni ADABIMA na KIKOBA.

Katika hotuba yake , Mheshimiwa Rais alisisitiza umuhimu wa Maonyesho ya SABASABA katika kuleta maendeleo ya kiuchumi. Alisema, “Maonyesho ya SABASABA ni kielelezo cha ustawi na maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Yanathibitisha moyo wa ujasiriamali na ubunifu wa Watanzania Kwa kuzileta pamoja biashara kutoka sekta mbalimbali, na kuwa maonyesho haya hayaoneshi tu uwezo wa kiuchumi bali pia yanachochea ushirikiano wa pamoja unaowezesha ukuaji wa uchumi.

Maonyesho ya SABASABA yanaendelea kuwa kilele cha maendeleo ya kibiashara nchini, yanatoa fursa kwa sekta mbalimbali kujumuika pamoja wakiwafikia wateja na wadau mbalimbali ambapo Ushiriki wa TCB katika maonyesho haya unathibitisha dhamira yake kushiriki katika ukuaji wa uchumi na ujumuishi wa kifedha.

ADABIMA ni mpango wa utoaji dhamana wa ada ambao TCB imeshirikiana na kampuni ya Metro Life Assurance ili kuwapa wazazi na walezi utulivu wa kiakili ambapo Mpango huo unahakikisha kwamba watoto wanaweza kuendelea na elimu yao hata pale wazazi au walezi wao wanapofariki au kupata ulemavu wa kudumu, na hivyo kulinda malengo yao ya kitaaluma.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki, Francis Kaaya, amesema, “Tunatambua umuhimu mkubwa wa elimu katika kujenga kesho bora ya jamii yetu na kwamba ADABIMA inawapa usalama wa kifedha lakini pia inalea ndoto na matarajio ya wateja wake na kufafanua kuwa, “Bidhaa hii ni uthibitisho tosha wa dhamira ya TCB Benki ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kadiri ya mahitaji yao na kuwahudumia Watanzania wote kwa ujumla.”

Kwa upande wake, Pray Henry Matiri, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Bidhaa za Kidigitali (Digital Product Operations Officer) ameeleza kuwa, “Kikoba ni zaidi ya fursa ya kidigitali, kwani Kikoba inabeba dhana pana ya uwazi, ujumuishi, na usalama katika uwekaji wa akiba na usimamizi bora wa kifedha.

KIKOBA ni bidhaa mpya, rahisi na yenye ufanisi ya kuweka akiba mtandaoni inayoboresha dhana ileile inayotumika katika vikundi vilivyozoeleka vya kuweka akiba na kukopeshana ,Bidhaa hii ya kidigitali na ya kifedha, ikiwezeshwa na ushirikiano wa kimkakati ambao TCB ilifanya na kampuni za simu nchini, inawawezesha wateja kusimamia fedha zao kwa urahisi kutoka viganjani mwao

Maonesho hayo ya biashara ya 48 yameanza tarehe 28 na ufunguzi rasmi ulifanyika rasmi 3 julai na Rais wa jamhuri ya msumbiji Filipe Jacinto Nyusi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ambapo zaidi ya nchi 26 zinashiriki na watu zaidi ya elf3 watashiriki na mwaka huu mamlaka ya maendeleo ya biashara Tantred imesema washiriki wameongezeka zaidi ukilinganisha na mwaka jana.














About the author

mzalendoeditor