Featured Kitaifa

HAMISA MOBETO ATOA POVU KISA WAANDAAJI WA SHOO

Written by mzalendoeditor

MWANAMITINDO, Msanii wa muziki na Bongo Movies Hamisa Mobeto,amesema  kuwa, huwa anachukizwa na baadhi ya watu kudharau kazi za watu wengine huku akisema kama ikitokea mtu akamfanyia hivyo wataishia kugombana.

Hamisa anasema kuwa, unaweza ukakuta mtu anakuita kwa ajili ya kwenda kufanya shoo ila ikifikia kwenye sehemu ya kutaja kiasi cha pesa, ukisema pesa kuwa tu hapo ujue ndiyo kwaheri huitwi tena.

“Hivi mtu unamuombaje msanii aje kufanya shoo, halafu akikupa bei yake unamjibu wasanii tunao wengi, vitu vingine bana, sasa si uwafuate hao wengi, huwa sipendezwi kabisa na mambo kama haya ndiyo maana mimi kwenye muziki nafanya kama kipaji wala sina muda wa kuhangaika na shoo maana najua kunilipa watanishindwa, tutaishia kugombana tu,” anasema Hamisa.

chanzo:Global 

About the author

mzalendoeditor